Pata taarifa kuu
PALESTINA-SIASA-USALAMA

Wapalestina wakubaliana kufanya uchaguzi mwaka 2018

Baada ya siku mbili ya mazungumzo mjini Cairo, makundi ya Waplestina yametangaza mkataba mpya kwa lengo la maridhiano. Baada ya miaka kumi ya uhasama na mgawanyiko, wamekubaliana kufanya uchaguzi wa wabunge na urais mwishoni mwa mwaka 2018.

Khalil al-Hayya, kiongozi wa Hamas, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kando na mazungumzo kati ya Wapalestina Cairo tarehe 22 Novemba 2017.
Khalil al-Hayya, kiongozi wa Hamas, wakati wa mkutano na waandishi wa habari kando na mazungumzo kati ya Wapalestina Cairo tarehe 22 Novemba 2017. MOHAMED EL-SHAHED / AFP
Matangazo ya kibiashara

Lakini mkataba huu mpya unaomba kujadili tena kwa kina mambo muhimu ya utata kati ya Hamas na Fatah, vyama viwili vikuu nchini Palestina.

Tarehe itatolewa na rais wa Mamlaka ya Palestina lakini muda wa mwisho hatimaye umewekwa: makundi ya Wapalestina yamekubaliana kufanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka 2018.

Uchaguzi huu utakuwa wa kwanza kufanyika katika maeneo yote ya Palestina tangu mwaka 2006. Leo hakuna tena vikao vya bunge - taasisi muhimu ya nchi kwa Malamlaka ya palestina na muhula wa rais ulimalizika mwaka 2009. Kufanyika kwa uchaguzi huo itakua ni hatua kubwa baada ya miaka kumi ya uhasama.

Lakini tamko la mwisho la kikao hicho kipya cha mazungumzo kimeomba, kwa mara nyingine tena, masuala nyeti zaidi yajadiliwe. Tamko hilo halikutaja hatma ya makundi ya waasi na usimamizi wa usalama katika Ukanda wa Gaza. Mkataba huo unatoa wito tu "kuondoa vizuizi vyote vinavyozuia jitihada za serikali kwa kutekeleza majukumu yake."

Mazungumzo yataendelea kati ya vyama vikuu viwili: Hamas na Fatah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.