Pata taarifa kuu
PALESTINA-USHIRIKINAO-MARIDHIANO

Serikali ya Palestina yakutana Gaza, mara ya kwanza toka mwaka 2014

Serikali ya Palestina imekutana katika Ukanda wa Gaza leo Jumanne, mara ya kwanza toka mwaka 2014 kwa lengo la kurejesha Mamlaka ya Palestina inayotambuliwa kimataifa.

Waziri Mkuu wa Palestina Rami Hamdallah (katikati), alipofika Beit Hanoun, tarehe 2 Oktoba 2017 katika Ukanda wa Gaza.
Waziri Mkuu wa Palestina Rami Hamdallah (katikati), alipofika Beit Hanoun, tarehe 2 Oktoba 2017 katika Ukanda wa Gaza. AFP
Matangazo ya kibiashara

Ukanda wa Gaza ni eneo lilil chini ya udhibiti wa kundi la Hamas, amearifumwandishi wa shirika la habari la AFP.

Kikao hiki cha Baraza la Mawaziri pia kitaonyesha maendeleo ya maridhiano kati ya Serikali ya Palestina na kundi la Hamas baada ya miaka 10 ya mgogoro mkubwa.

Licha ya kushindwa kwa jaribio la awali la kuunganishwa kwa eneo hilo kuwa chini ya Mamlaka ya Palestina, ziara ya viongozi wa Palestina ilianza siku ya Jumatatu katika ukanda wa Gaza kiongozwa na Hamdallah. Ziara hii ambayo ni ya kwanza tangu mwaka 2015, itaandaa hatua ya kukabishi mamlaka kwa viongozi wa palestina kutoka mikononi mwa kundi la Hamas.

Hamas iliiangusha madarakani Mamlaka ya palestina katika Ukanda wa Gaza mwaka 2007 na kuanzisha vita vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kundi hili na Fatah, hasimu wake mkuu anayetawala sehemu kubwa ya nchi ya Palestina.

Tangu wakati huo Mamlaka ya Palestina inaendesha mamlaka yake madogo katika Ukingo wa Magharibi peke, unaokaliwa na Israel kwa miaka 50 kutoka kilomita chache na Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.