Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-IRAN-UTURUKI-USALAMA

Putin kukutana na marais wa Uturuki na Iran kuzungumzia mgogoro wa Syria

Mkutano kuhusu mchakato wa amani nchini Syria unatazamiwa kufanyika Sochi, nchini Urusi, leo Jumatano, 22 Novemba. Mkutano huu ni kati ya wadhamini watatu wa mchakato wa Astana: Urusi,Uturuki na Iran.

Siku moja kabla ya mkutano kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Syria, rais wa Urusi Vladimir Putin alimpokea mwenzake wa Syria, Bashar Al Assad, Sochi Novemba 20, 2017.
Siku moja kabla ya mkutano kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Syria, rais wa Urusi Vladimir Putin alimpokea mwenzake wa Syria, Bashar Al Assad, Sochi Novemba 20, 2017. Sputnik/Mikhail Klimentyev/Kremlin via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin anataka kushawishi wenzake wawili, Recep Tayyip Erdogan na Hassan Rohani kusaidia jitihada za kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro wa Syria. Na kuandaa mkutano nchini Urusi kati ya upinzani wa utawala wa Bashar al Assad na serikali.

Hili ni lengo kubwa la kidiplomasia la Vladimir Putin kukutana katika mji wa Sochi na wawakilishi wa upinzani na serikali ya Syria. Mkutano huo utakuwa na lengo la kuunda katiba mpya ya Syria na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa kwa mgogoro nchini humo tangu mwaka 2011. Mradi huu ulioitwa "National Dialogue Congress" (mkutano wa mazungumzo ya kitaifa) utarejesha imani kwa Urusi ambayo imekua ikishtumiwa kuchochea mgogoro wa Syria.

Lakini ili kufikia hatua hiyo, Vladimir Putin atalazimika kushawishi Iran na Uturuki kumuunga mkono katika mradi huo.

Urusi inataka kutoa mwaliko kwa Wakurdi kutoka Syria kushiriki mazungumzo, huku Uturuki ikipinga jambo hilo. "Tumeona kwamba Erdogan hakubali msimamo wa Urusi kuhusu Wakurdi. Lakini kwa upande wa Erdogan, suala la Wakurdi limekuwa kipaumbele chake. Ukweli ni kwamba Urusi haiko tayari kuachana na Wakurdi, haitaki kupoteza mawasiliano ambayo imeanzisha nao. Kwa hiyo viongozi hawa wawili watahitaji kupata suluhisho, "anasema Alexandre Choumiline, mkurugenzi wa Kituo cha Uchambuzi wa Migogoro Mashariki ya Kati.

Pia kuna tofauti nyingine inayojitokeza kabla ya makubaliano ya mradi huo. "Tatizo ni uwepo wa askari wa Iran nchini Syria. Hivi sasa, Saudi Arabia na Marekani wanashinikiza Urusi ili iweze kuhakikisha kama Iran itaondoa askari wake wote au la nchini Syria. Na ni wazi Iran haiwezi kukubali kufanya hivyo, " ameongeza Bw. Choumiline.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.