Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-HAKI

Ruhsa kwa wanawake kuendesha gari Saudi Arabia

Saudi Arabia, nchi moja pekee duniani ambayo ilikua ikikataza wanawake kuendesha gari hatimaye imewaruhusu, kulinganana agizo la Mfalme wa nchi hiyo lililotolewa siku ya Jumanne.

Mwanamke akiendesha gari nchini Saudi Arabia, nchi pekee duniani imekua ikipiga marufuku kwa wanawake kuendesha gari.
Mwanamke akiendesha gari nchini Saudi Arabia, nchi pekee duniani imekua ikipiga marufuku kwa wanawake kuendesha gari. REUTERS/Faisal Al Nasser
Matangazo ya kibiashara

Mfalme Salmane alitoa agizo la "kuruhusu kupewa leseni bila kujali kwa wanaume na wanawake," linaeleza agizo lililochapishwa na shirika la la habari la serikali la SPA.

Hatua hii, ambayo wanaharakati wamekua wakidai na hata kufungwa kwa kudharau marufuku hayo, itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Juni mwaka wa 2018 katika katika nchi hii ya Ghuba.

Huu ni uamuzi wa kihistoria nchini Saudi Arabia.

"Ninashtuka, ninafurahi sana," amesema mjini Riadh Haya Rakyane, mfanyakazi wa benki mwenye umri wa miaka 30. "Sikuweza kutarajia uamuzi huo kabla ya miaka 10 au 20," aliliambia shirika la habari la AFP.

"Ni siku ya furaha sana! Sijaamini hivyo bado, Siamini kabla ya kuona kwa macho yangu mwenyewe," amesema kwa upande wake Chatha Dousri akiliambia shirika la habari la AFP.

Wanawake wengi kutoka Saudi Arabia ambao wanaweza kuendesha gari London au Dubai lakini hapana Riadh walijaribu kusisitiza kuondolewa kwa marufuku haya nchini Saudi Arabia lakini walikamatwa.

Marekani ilijibu vyema kwa uamuzi wa mshirika wake mkubwa katika ukanda wa Mashariki ya Kati kwa kuruhusu wanawake kuendesha gari, huku rais Donald Trump akisema ni "hatua chanya kwa kuendeleza haki za wanawake nchini Saudi Arabia."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, pia amekaribisha uamuzi huo wa Saudi Arabia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.