Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-USALAMA

Usalama waimarishwa wakati ibada ya Hija ikianza Saudi Arabia

Miji mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina inawapokea Waislamu zaidi ya milioni mbili ikiwa Jumatano hii ni siku ya kwanza ya ibada hiyo.

Vikosi vya  usalama mbele ya mitambo ya ukaguzi, Makka tarehe 29 Agosti 2017.
Vikosi vya usalama mbele ya mitambo ya ukaguzi, Makka tarehe 29 Agosti 2017. REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Katika ibada hii Wairani ambao walikua walipigwa marufuku kuingia katika nchi hiyo ya Kiislamu kutoka madhehebu ya Sunni, hatimaye wameruhusiwa kufanya ibada hiyo katika mji mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina.

Mwaka jana Wairan hawakuweza kwenda Makka kufuatia mivutano ya kisiasa kati ya Tehran na Riyadh. Usalama wa mahujaji ni moja ya changamoto ya ibada hii.

Mamlaka nchini Saudi Arabia inasema imetenga kikosi cha polisi 100,000 mwaka huu, lakini pia wafanyakazi 17,000 wa ulinzi wa raia na magari ya wagonjwa zaidi ya mia moja. Nchi hiyo ya kifalme imeahidi kutoa ulinzi wa kutosha kwa mahujaji kutoka nchi 80.

Saudi Arabia inataka kuepuka ajali yoyote hasa tukio jipya la mkanyagano. Matukio mabayayalitokea mara kadhaa katika miongo ya hivi karibuni katika mji wa Makka ambapo watu 2,300 walipoteza maisha muaka miili iliyopita kulingana na takwimu za serikali.

Matukio mengine ya hatari huenda yakashuhudiwa katika ibada hii ya Hija: shambulio la kigaidi au magonjwa ya kuambulia. Mnamo mwaka 2009, virusi vya mafua ya ndege A vilizua hali ya sintofahamu nchini Saudi. Mwaka huu, janga la kipindupindu nchini Yemen linatia wasiwasi kwa huduma za afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.