Pata taarifa kuu
IRAN-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Wairani waruhusiwa kufanya Hija Makka licha ya mvutano na Saudi Arabia

Waislamu zaidi ya milioni mbili kutoka duniani kotewameanza Jumatano hii ibada kubwa ya Hija katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia. Maelfu ya Wairani tayari wamewasili nchini Saudi Arabia, wakati ambapo Tehran na Riyadh bado wanavutana na uhusiano wa kidiplomasia haujarejeshwa.

Waumini wakiswali katika Msikiti Mkuu wa Makka ikiwa ni mwanzo wa ibada kubwa ya Hija tarehe 29 Agosti 2017.
Waumini wakiswali katika Msikiti Mkuu wa Makka ikiwa ni mwanzo wa ibada kubwa ya Hija tarehe 29 Agosti 2017. REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo, safaru za ndege zimeruhusiwa kati ya Saudi Arabia na Iran kwa minajili ya kuendesha ibada kubwa ya Hija, ambayo ni nguzo ya tano ya imani kwa Uislamu. Visa zimetolewa kwa njia ya mtandao.

Saudi Arabia haina tena ubalozi nchini Iran kwa ajili ya kutoa visa na ilipiga marufuku safari za ndege na Iran. Riyadh ilivunja mahusiano na Tehran baada ya mashambulizi na uvamizi katika ubalozi wake mnamo mwezi Januari mwaka 2016.Vitendo ambavyo vilitekelezwa na umati wa watu wenye hasira ambao walifanya hivyo kutokana na uamuzi wa Saudi Arabia wa kumyonga kiongozi wa kidini wa Kishia.

Mwaka 2016, mahujaji wa Iran hawakuruhusiwa kushiriki Hija, nchi hizo mbili hazijaweza kutatua migogoro yao, hasa katika suala la usalama wa mahujaji. Mwaka 2015, watu 2,300 ikiwa ni pamoja na Wairani 464, walipoteza maisha katika kukanyagana.

Hatimaye, baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo, Riyadh imeruhusu safari za ndege za Iran na kuruhusu sehemu ya mahujaji wa Iran kusafirishwa kwa ndege za shirika la ndege la Saudi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.