Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-USALAMA

Mami ya raia wayahama makazi yao kufuatia mapigano Saudia

Eneo la Mashari ya Saudi Arabia linaendelea kukumbwa na mapigano kati ya jeshi la nchi hiyo na watu wenye silaha. Maafisa kadhaa wa polisi na watu waliojihami wameuawa katika mpigano ya hivi karibuni.

Waandamanaji kutoka Iran wakati wa maandamano ya kulaani kunyongwa kwa Sheikh Al- Nimr na Saudi Arabia, Januari 3, 2016, Tehran.
Waandamanaji kutoka Iran wakati wa maandamano ya kulaani kunyongwa kwa Sheikh Al- Nimr na Saudi Arabia, Januari 3, 2016, Tehran. REUTERS/Raheb Homavandi/TIMA ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya wakazi wa eneo hilo wamelazimika kuyatoroka makazi yao kutokana na mapigano yaliyoanza tangu wiuki kadhaa zilizopita.

Vikosi vya usalama vimelenga maeneo ya kale ya Awamiya, ambayo wanasema ni sehemu wanakojificha wapiganaji wa Shia.

Maafisa wa utawala wanataka kulibomoa eneo hilo la kale lenye miaka 200 katika operesheni ilioanzishwa mnamo mwezi Mei.

Mji wa Awamiya ni nyumbani anakotoka Sheikh Nimr al-Nimr, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi anayewaunga mkono waandamanaji wa Kishia, ambaye aliuawa mwaka mmoja na nusu uliopita.

Sheikh Nimr al-Nimr, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi anayewaunga mkono waandamanaji wa Kishia, ambaye aliuawa mwaka mmoja na nusu uliopita.
Sheikh Nimr al-Nimr, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi anayewaunga mkono waandamanaji wa Kishia, ambaye aliuawa mwaka mmoja na nusu uliopita. REUTERS/Saudi Press Agency

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.