Pata taarifa kuu
IRAQ-ISIL

Shambulio jingine latekelezwa Baghdad ndani ya saa 24

Kumetokea mlipuko wa pili jijini Baghdad nchini Ira na kuua watu wanaokadiriwa kufikia 8 na kujeruhi wengine zaidi ya 30.

Polisi mjini Baghdad wakikagua moja ya gari lililotumiwa kujitoa muhanga na wanajihadi wa kiislamu wa ISIL hivi karibuni
Polisi mjini Baghdad wakikagua moja ya gari lililotumiwa kujitoa muhanga na wanajihadi wa kiislamu wa ISIL hivi karibuni REUTERS/Khalid al-Mousily
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huu kwenye daraja la Al-Shahada limetokea ikiwa ni saa chache tu zimepita baada ya mtoaji muhanga mmoja kujilipua akitumia gari kwenye wilaya ya Karrada na kuua watu zaidi ya 27 na kujeruhi wengine zaidi ya 100.

Vyombo vya usalama nchini Iraq vinasema kuwa shambulio hili la pili pia limetekelezwa kwa kutumia gari.

Kundi la Islamic state nchini Iraq na lile la Levant wamekiri kuhusika na shambulio la kwanza ambalo limetokea wakati huu waumini wa dini ya kiislamu wakiendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Mashambulizi yote mawili yametokea katika kipindi cha mfungo wa Ramadan ambapo mamia ya watu huchelewa kulala na wengine hula kwenye migahawa kujiandaa na mfungo wa siku inayofuata.

Hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika kwenye shambulizi la pili licha ya kuwa vyombo vya usalama vina amini kuwa ni wapigajani wa kijihadi wa Islamic State.

Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan mwaka jana mji wa Karrada ulishuhudia mashambulizi mfululizo ambapo watu zaidi ya 300 waliuawa ikiwa ni shambulio baya zaidi kutekelezwa kwenye jiji kuu la Iraq.

Shambulio lile pia kundi la Islamic State nchini Iraq lilikiri kuhusika.

Kundi la ISIL limetoa taarifa kuthibitisha wapiganaji wake kuhusika kwenye shambulio la kwanza walilosema linawalenga waumini wa madhehebu ya Kishia.

IS inawachukulia waumini wa Kishia wanawake, wanaume na watoto kama wafuasi wa elimu ya magharibi na wasaliti na hivyo wanastahili kushambuliwa.

Picha za kwenye mtandao zinaonesha madhara yaliyosababishwa na shambulio hili ambalo lililenga watu waliokuwa kwenye mgahawa mmoja wakinunua Ice Cream.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.