Pata taarifa kuu
IRAQ

Maelfu ya raia wa Iraq waendelea kuukimbia mji wa Mosul, hali yazidi kuwa mbaya

Mamia ya raia wamekimbia mji wa Mosul kupitia maeneo ya jangwa, wakikwepa mapigano kati ya vikosi vya Serikali na wapiganaji wa Islamic State kwenye mji huo, wakiungana na maelfu ya raia wengine waliokimbia nyumba zao kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya magharibi mwa mji huo nchini Iraq.

Vikosi vya Iraq vikiwa kwenye sehemu ya operesheni kwenye mji wa Mosul.
Vikosi vya Iraq vikiwa kwenye sehemu ya operesheni kwenye mji wa Mosul. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Iraq vimeanzisha kampeni kali Februari 19 mwaka huu na kufanikiwa kulikamata tena eneo la magharini mwa mji wa Mosul kutoka kwa wapiganaji wa ISIL, ambapo waliuchukua uwanja wa ndege na kusonga mbele kuelekea kaskazini.

Vikosi hivyo vimefanikiwa kufika eneo la kusini mwa mji huo ambako madaraja makubwa yameharibia kupitia mto Tigris, hatua ambayo itaviruhusu vikosi hivyo kutengeneza madaraja ya muda kati ya eneo hilo na eneo la magharibi mwa mji wa Mosul.

Lakini hata hivyo licha ya vikosi vya Iraq kufanikiwa kuunganisha eneo la ukingo wa mashariki na magharibi mwa mji wa Mosul, mapigano makali bado yako mbele yao na raia wamekuwa wakinaswa kwenye mapigano hayo.

Kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu yanayotoa msaada kwa raia wanaokimbia mji huo, wanasema kuwa raia wengi waliokimbia wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu.

Hata hivyo vikosi vya Serikali vimekuwa vikifanya upekuzi wa hali ya juu kwa wanaume wanaokimbia mji huo, huku wakiwatenganisha na wanawake ambao nao hutenganishwa kwa hofu kuwa huenda wapiganaji wa Islamic State wakatumia mwanya huo kutekeleza mshambulizi ya kujitoa muhanga kama wanavyofanya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.