Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya amani juu ya Syria yazinduliwa Jumatatu mjini Astana

Mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya serikali ya Damascus na wapiganaji wa waasi yanaanza Jumatatu hiiJanuari 23 katika mji wa Astana, nchini Kazakhstan. Mazungumzo haya yanafadhiliwa na Urusi, Uturuki na Iran.

Baada ya miaka 6 ya vita na zaidi ya watu 300,000 kupoteza maisha, serikali ya Syria inaaza mazungumzo na makundi ya waasi mjini Astana, Jumatatu Januari 23, 2017.
Baada ya miaka 6 ya vita na zaidi ya watu 300,000 kupoteza maisha, serikali ya Syria inaaza mazungumzo na makundi ya waasi mjini Astana, Jumatatu Januari 23, 2017. REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya ni ushindi wa kidiplomasia kwa Urusi ambayo iliishawishi Uturuki kujiondoa katika msimamo wake wa kutaka Bashar Al Assad aondoke, na kuitenga Marekani katika mchakato huo, ingawa utawala mpya wa Marekani ulikua umealikwa.

Kazakhstan, ambayo ni sehemu ya zamani ya jamhuri ya Urusi katika Asia ya Kati, yenye Waislamu wengi na wanaozungumza Kituruki, inaweza ka shingo upande kukataa kuwa mwenyeji wa mkutano huu, ametathmini mwandishi wa RFI mjini Moscow, Muriel Pomponio.

Urusi ndio inasimamia mazungumzo haya na tayari imezishawishi pande zote zinatakazoshiriki mazungumo kukubali Rais Bashar Al Assad aendelee kusalia madarakani kama rais wa Syria. Tayari Uturuki umelegeza msimamo na kukubali hoja ya Urusi. Hivi karibuni afisa mmoja wa Uturuki alitangaza kwamba kwa sasa Uturuki haiko tayari kumtaka Bashar Al Assad kuachia ngazi.

Baada ya kushindwa katika mji wa Aleppo, makundi ya waasi kwa sasa hayana nguvu katika uwanja wa vita. Mdhamini wao ambaye ni Uturuki hatimaye amejiunga na Urusi, na nchi za Kiarabu hazitashirika katika mazungumzo hayo yanayotazamiwa kuanza Jumatatu hii mjini Astana.

Serikali ya Syria imewataka waasi kuweka chini Silaha na kujisalimisha, ikiwa na imani kwamba maeneo yote yaliyo chini ya udhibiti wa waasi, hivi karibuni yatakua chini ya himaya ya jeshi la serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.