Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-USALAMA

Urusi kuondoa ndege zake nchini Syria

Urusi imeanza zoezi la kuwaondoa wanajeshi wake na ndege zake za kivita kutoka nchini Syria. Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya kufikia mkataba na Uturuki kusitisha mapigano nchini humo.

Wanajeshi wa jeshi la Syria mjini Aleppo Desemba 21, 2016.
Wanajeshi wa jeshi la Syria mjini Aleppo Desemba 21, 2016. GEORGE OURFALIAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwaka 2015, jeshi la Urusi limekuwa likiisaidia Syria kuwashambulia waasi ambao wamekuwa wakipambana na uongozi wa rais Bashar Al Assad.

Kuanza kuondoka kwa wanajeshi wa Syria pia kunaelezwa kuashiria kushindwa kabisa kwa waasi ambao wameondolewa katika mji wa Allepo baada ya vita vya miaka mitano.

Urusi, Uturuki na Iran sasa zipo katika harakati za kutaka kufanyika kwa mazungumzo ya amani baadaye mwezi huu nchini Kazakhstan.

Hata hivyo, waasi wa upinzani wametishia kutoshiriki katika mazungumzo hayo na serikali ya rais Assada, kwa madai ya kuvunjwa kwa mkataba wa kusitisha vita nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.