Pata taarifa kuu
IRAQ-UTURUKI-MVUTANO

Vita vya Mosul: mvutano kati ya Uturuki na Iraq

Uturuki imechukua msimamo mgumu katika mgogoro huu, hasa kwa sababu serikali ya Iraq inapinga kushiriki kwa jeshi la Uturuki katika vita hivi, Jambo ambalo Uturuki imefutilia mbali.

Vikosi vya usalama vya Iraq mashariki mwa mji wa Mosul, Iraq, Oktoba 19, 2016.
Vikosi vya usalama vya Iraq mashariki mwa mji wa Mosul, Iraq, Oktoba 19, 2016. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Askari wengi wa Uturuki wapo katika ardhi ya Iraq, wakufunzi kutoka nchi hiyo kwa sasa wapo katika kambi moja kwenye umbali wa kilomita kadhaa kutoka mji wa Mosul ambao wanatoa mafunzo kwa watu wanaojitolea hasa kutoka jamii ya Wasunni. Lakini uwepo huu wanajeshi wa Uturuki katika ardhi ya Iraq unapingwa na serikali ya Iraq, ambayo imetaja kitendo hicho kuwa ni 'udhibiti wa kimabavu', na kuomba kikosi hiki kuondoka haraka iwezekanavyo.

Mvutano kati ya madhehebu ya kidini

Hali hii ya mvutano na serikali ya Baghdad pia inaonyesha mvutano wa madhehebu ya kidini. Uturuki inajiandalia hasa kuudhibiti mji wa Mosul baada ya vita. Uturuki inataka kuhakikisha kwamba wanamgambo Wakishia sawa na wapiganaji wa kikurdi wa PKK wasithubuti kuchukua udhibiti wa Mosul, mji ambao una historia muhimu kwa Uturuki. Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi Uuruki, mji huo ulikua eneo la Uturuki, lakini baada ya Vita Kuu vya Dunia Uturuki ililipoteza eno hilo na kuwa upande wa Iraq.

Uturuki pia imekua kama mlinzi wa watu kutoka jamii ya Wasuni katika ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.