Pata taarifa kuu
IRAQ-IS

Jeshi la Iraq lajaribu kuuteka mji wa Qayyarah

Jumanne hii Agosti 23, 2016 jeshi la Iraq limeanzishamashambulizi katika kujaribu kuuweka kwenye himaya yake mji wa Qayyarah, kilomita 60 kutoka mji wa Mosul, ngome ya kundi la Islamic State nchini Iraq.

Vikosi vya usalama vya Iraq karibu na mji wa Qayyarah, Iraq, Agosti 15, 2016.
Vikosi vya usalama vya Iraq karibu na mji wa Qayyarah, Iraq, Agosti 15, 2016. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Mosul, hata hivyo unachukuliwa kama hatua ya mwisho kabla mji mkuu uliyotangazwa na kundi la IS.

Vikosi vya Iraq vimeingia Jumanne hii katika mji wa Qayyarah, kusini mwa mji wa Mosul. Mji wa Qayyarah unadhibitiwa kwa miaka miwili sasa na kundi la Islamic State. Ni ni hatua ya mwisho kabla ya kuuteka mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq, Mosul.

Vikosi maalum vya Iraq wamejipa muda wa masaa sita kwa kuudhibiti mji wa Qayyarah. Baada ya kuanzisha mashambulizi, wanajeshi wamekabiliana na upinzani mkali licha ya mashambulizi ya usiku yaliyotekelezwa na muungano wa kimataifa.

Siku moja kabla, Jumatatu wiki hii, wapiganaji wa kundi la Islamic State waliendesha mashambulizi kadhaa kwa gesi ya klorini kwa kurudisha shambulio. Lakini Jumanne hii, jeshi la Iraq limefaulu kupata kuingia katikati ya mji huu wa Qayyarah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.