Pata taarifa kuu
SYRIA-IS-MAPIGANO

OSDH: mashambulizi manne ya anga yalenga maeneo ya waasi katika mji wa Aleppo

Mashambulizi manne ya anga yamelenga Jumapili hii maeneo yanayoshikiliwa na wa waasi katika mji wa Aleppo, kwa mara ya kwanza tangu kuanza kutekelezwa mkataba wa usitishwaji wa mapigano Jumatatu Septemba 12 kwa jitihada zaUrusi na Marekani, Shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH) limesema.

Uharibifu unaendelea kushuhudiwa katika mji wa Aleppo, Syria, kufuatia mapigano yanayoendelea.
Uharibifu unaendelea kushuhudiwa katika mji wa Aleppo, Syria, kufuatia mapigano yanayoendelea. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), watu kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulizi manee ya anganiyaliyolenga maeneo ya waasi katika mji wa Aleppo. Shirika hili ambalo lina mtandao mkubwa wa vyanzo nchini Syria, halikutoa maelezo mengine au kueleza ni akinanani waliohusika na mashambulizi hayo.

Urusi na Marekani wanasimamia mkataba wa usitishwaji wa mapigano ambao umeendelea kuwa tete. Mashambulizi ya Jumamosi usiku yaliyoendeshwa na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya ngome za jeshi la Syria katika eneo la Deir ez-Zor, kaskazini mwa nchi, yangelipsababisha mkataba wa usitishwaji wa mapigano unavunjika. Ikituhumiwa na serikali ya Damascus na Moscow, muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani, ulikkiri kushambulia kile ambacho ilidhani ni ngome ya kundi la Islamic State nchini Syria, na kukusem akusikitishwa na kitendo hicho.

Ni katika mji wa Aleppo, mji mkuu wa zamani wa kiuchumi wa Syria, ambapo mapigano yanaendelea kurindima. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imewashtumu waasi kwamba wamekua wakijiandaa kwa ajili ya mashambulizi makubwa dhidi ya jeshi la Syria. Moscow pia imekosoa Marekani kwa kutoheshimu ahadi zake zinazolenga kutenganisha "magaidi" na viosi vya upinzani nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.