Pata taarifa kuu
SYRIA-UTURUKI

Syria: jeshi la Uturuki na waasi waendelea mashambulizi yao

Mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhangayalifanyika katika miji mbalimbali nchini Syria na kundi la Islamic State Jumatatu Septemba 5. Mashambulizi hayo yanatokea wakati ambapo kundi hili la kijihadi linaendelea kupata pigo kubwa nchini Syria.

Wapiganaji wa kundi la waasi wa Syria la FSA linalopambana na serikalii, lakini pia liko upande wa jeshi la Uturuki katika eneo la kaskazini dhidi ya wapiganaji wa kijihadi na vikosi vya Kikurdi.
Wapiganaji wa kundi la waasi wa Syria la FSA linalopambana na serikalii, lakini pia liko upande wa jeshi la Uturuki katika eneo la kaskazini dhidi ya wapiganaji wa kijihadi na vikosi vya Kikurdi. REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Tukio la hivi karibuni: Uturuki na shirika la haki za binadamu nchini (OSDH) wanasema kundi la Islamic State lilitimuliwa katika mpaka wa Uturuki na Syria.

Waasi wa Syria wakiungwa mkono na jeshi la Uturuki kaskazini mwa Syria wanaendelea kusonga mbele kwa siku ya kumi na tatu sasa ya operesheni iliyobatizwa kwa jina la "ngao ya mto." Baada ya kudhibiti eneo la mpakani lililokua likishikiliwa na kundi la IS, sasa waasi hao wanapania kuanzisha mashambulizi yao kusini, katika mji wa al-Bab, ambapo wanajihadi walikimbia, ikiwa ni pamoja na mashariki, katika mji wa Minbej, ambapo kuna wapiganaji wa Kikurdi.

Hivi ndivyo anavyoeleza, Yaser Ibrahim, mjumbe wa kamati kuu ya kundi la Nureldine el-Zangi, linalopigana upande wa waasi wa Syria (FSA): "Vita vyetu kaskazini mwa Syria vinalenga kundi la IS, lakini pia makundi ya wapiganaji ikiwa ni pamoja na kundi la YPG. Hatua inayofuata ni ya safisha mji wa mashariki wa Aleppo hadi kwenye bwawa la Techrine. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.