Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-SYRIA

Marekani yakosa mweleko kufuatia mashambulizi ya Uturuki nchini Syria

Mashambulizi ya kijeshi ya Uturuki nchini Syria dhidi ya kundi la Islamic State, ambayo pia yanalenga kuzuia waasi wa Kikurdi wa Syria kusonga kwenye mpaka wake, yamesababisha Marekani kuwa kando kati ya mshirika wake Uturuki na waasi wa Kikurdi ambao inawafadhili.

Msururu wa vifaru vya jeshi la Uturuki vikielekea kwenye mpaka wa Syria karibu na mji wa Karkamis.
Msururu wa vifaru vya jeshi la Uturuki vikielekea kwenye mpaka wa Syria karibu na mji wa Karkamis. BULENT KILIC / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wiki tano baada ya mapinduzi yaliyoshindwa na maombi ya mara kwa mara ya serikali ya Ururuki ili Marekani imrejeshe Imam wa zamani Fethullah Gulen, kuingilia kijeshi kaskazini mwa Syria kunaweza kuchochea hali ya sintofahamu katika mahusiano kati ya Marekani na Uturuki, ambayo tayari yameingiliwa na dosari, wataalam wameonya.

Kwa sababu katika vita vya Syria, ambavyo vimekua na ugumu zaidi na kuingiliwa kimataifa, Marekani inasaidia kundi kuu la wanamgambo wa Kikurdi wa chama cha PYD na tawi lake la kijeshi la YPG.

Hata hivyo Uturuki inapigana dhidi ya Wakurdi katika ardhi yake na haitaki kuona Wakurdi wa Syria wanapanua eneo lake kwenye mpakani wake.

Kwa upande wa Uturuki, chama cha PYD na tawi lake la kijeshi la YPG ni makundi ya "kigaidi", kama vile chama cha kikurdi cha PKK, kundi la wapiganaji lililoanzishwa tangu mwaka 1984 nchini Uturuki. Kwa upande wa Marekani chama cha PKK ni kundi la "kigaidi", lakini hapan chama cha PYD na tawi lake la kijeshi YPG.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.