Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI

Syria: mazungumzo kati ya Moscow na Washington yashindikana

Marekani na Urusi wameshindwa kukubaliana Jumatatu hii kuhusu Syria wakati wa mazungumzo katika mkutano wa G20 mjini Hangzhou (Mashariki mwa China), kwa sababu ya tofauti zinazoendelea, amesema mwanadiplomasia wa Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,  John Kerry (kushoto) na Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia) Agosti 26, 2016.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry (kushoto) na Waziri wa mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia) Agosti 26, 2016. REUTERS/Martial Trezzini/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo mapya ya Jumatatu hii kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, yamemalizika bila ya kufikia makubaliano, kwa mujibu wa mwanadiplomasia wa Marekani.

Jumapili hii Agosti 4, Washington ilishtumu Moscow kurejelea baadhi ya masuala katika mazungumzo hayo, na uweka ugumu kwa sasa mkataba wa ushirikiano kati ya mataifa haya mawili makubwa.

Urusi na Marekani, ambao wanaendelea na mashambulizi tofauti dhidi ya wapiganaji wa kijihadi nchini Syria hawaafikiani juu ya hatima ya rais wa Syria Bashar al-Assad, wakati ambapo serikali ya Damascus inaendelea kulenga upinzani wa Syria kwa msaada wa Urusi, tofauti nyingine na Marekani.

Rais wa Marekani Barack Obama na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wanatazimiwa kukutana Jumatatu hii, lakini kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia,ni vigumu kuafikia makubaliano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.