Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-TALIBAN

Mullah Haibatullah ateuliwa kiongozi mpya wa Taliban

Wapiganaji wa kundi la Taliban nchini Afghanistan wamemteua kiongozi wao mkuu mpya. Siku nne baada ya kifo cha Mullah Mansour katika shambulio la anga la Marekani katika ardhi ya Pakistan, mmoja wa wasaidizi wake, Haibatullah Mullah amemrithi.

Picha isiyo kuwa na tarehe ya kiongozi mpya wa Taliban.
Picha isiyo kuwa na tarehe ya kiongozi mpya wa Taliban. AFP
Matangazo ya kibiashara

Haibatullah Akhundzada alikuwa hadi Jumamosi iliyopita msaidizi wa Mullah Mansour. Mullah Haibutullah, muhubiri mkuu, ambaye kama watangulizi wake wawili ni kutoka katika mkoa wa Afghanistan wa Kandahar. Ameteuliwa kwa makubaliano na baraza kuu la Taliban, lililokutana tangu Jumapili Mei 22 katika eneo la siri pengine karibu na mji wa Quetta, nchini Pakistan.

Mullah Haibatullah, mwenye umri ulio karibu na hamsini, ameteuliwa badala ya mtotot wa Mullah Omar, kiongozi wa kihistoria, mwasisi wa kundi la Taliban na kiongozi wa juu wa kundi la Haqqani, mtetezi wa kijeshi katika safa ya mbele.

Kiongozi huyu mpya wa kundi la waasi wa Taliban alikuwa mkuu wa mahakama za wapiganaji wa kundi la Taliban tangu kutimuliwa mamlakani mjini Kabul mwaka 2001. Ni mmoja miongoni mwa viongozi waanoaminika katika shughuli za kigaidi za kundi la waasi wa Taliban. Ni mhubiri mwenye ushawishi mkubwa katika uongozi wa shule kubwa ya kidini (Madrasa), inayopatikana katika mkoa wa Baluchistan ambapo Mullah Mansur aliuawa na shambulio la ndege ya Marekani isio na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.