Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI-SYRIA-USHIRIKIANO-USALAMA

Syria: Moscow na Washington waongeza shinikizo kwa kusitisha mapigano

Urusi na Marekani wameongeza shinikizo Jumatano hii kwa washirika wao katika vita nchini Syria ili kutekeleza kwa makataba wa usitishwaji mapigano unaotazamiwa kuanza kutekelezwa Jumamosi wiki hii.

Askari wa jeshi la serikali ya Syria wakisherehekea baada ya kukiteka Kijiji cha Ratian, kaskazini ya jimbo la Aleppo, Februari 6, 2016.
Askari wa jeshi la serikali ya Syria wakisherehekea baada ya kukiteka Kijiji cha Ratian, kaskazini ya jimbo la Aleppo, Februari 6, 2016. AFP / GEORGE OURFALIAN
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo hakuna imani yoyote kwamba mkataba huo utatekelezwa kufuatia jinsi ilivyo. Hali ni tete katika uwanja wa vita.

Usitishwaji huo wa mapigano bado uko matatani kwani makundi muhimu ya wanajihadi ya Islamic State (IS) na Al-Nosra Front (tawi la Al Qaeda nchini Syria) ambayo yanadhibiti maeneo makubwa ya ardhi ya Syria na ambayo yanalengwa na mashambulizi ya jeshi likisaidiwa na mashambulizi ya anga ya Urusi pamoja na mashambulizi ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Katika mgogoro huo mkubwa ambao unadumu karibu miaka mitano, Urusi na Iran wanaunga mkono utawala wa Bashar al-Assad wakati ambapo Marekani, Saudi Arabia na Uturuki wakiunga mkono waasi wa Syria na mkataba wa usitishwaji mapigano utatekelezwa kwa makundi haya makuu mawili.

Lakini waasi wanaonekana kuwa ni wadhaifu dhidi ya kuongezeka kwa nguvu za makundi ya kijihadi na ambayo yametengwa katika mchakato huo nchini Syria. Hata hivyo utawala umeendelea kuyarejesha kwenye himaya yake baadhi ya maeneo baada ya msaada wa Urusi.

Jumatano hii, Urusi imetangaza kuwa Rais Bashar Al-Assad amethibitisha kuwa yuko "tayari kuchangia katika utekelezaji wa kusitisha mapigano", ambayo ameeleza "hatua muhimu kwa kuelekea katika ufumbuzi wa kisiasa," kulingana na taarifa iliyotolewa baada ya mazungumzo ya simu kati ya rais wa Syria na Vladimir Putin.

Hata hivyo, wawili hawa "wamesisitiza umuhimu wa mapambano dhidi kundi la IS, Al-Nusra Front na makundi mengine ya kigaidi yanayoonekana kuendeleza ugaidi na Umoja wa Mataifa," kwa mujibu wa Ikulu ya Kremlin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.