Pata taarifa kuu
SYRIA-MAZUNGUMZO

Damascus yakubali mkataba wa usitishwaji mapigano

Serikali ya Damascus Jumanne hii, imekubali rasimu ya Marekani na Urusi kuhusu mkataba wa usitishwaji mapigano, ambapo utekelezaji wake unaweza kukabiliwa na changa moto kubwa kama kutengwa kwa makundi ya kiislamu yenye ushawishi mkubwa.

Askari wa Syria wakikagua eneo kulikotokea milipuko miwili iliotokea Homs Jumapili Februari 21, 2016.
Askari wa Syria wakikagua eneo kulikotokea milipuko miwili iliotokea Homs Jumapili Februari 21, 2016. REUTERS/SANA
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huu, uliopangwa kuanza Jumamosi usiku wa manane saa za Syria (sawa na Ijumaa saa nne usiku saa za kimataifa), hauhusishi hasa makundi ya Islamic State (IS) na Al-Nosra Front, tawi la Al Qaeda nchini Syria, makundi ambayo yanadhibiti sehemu kubwa ya ardhi ya Syria.

Katika uwanja wa vita, waasi na raia wameonyesha wasiwasi wao kuhusu mkataba huo wa usitishwaji mapigano, wakiwa na mashaka juu ya nia njema ya serikali na washirika wake.

"Jamhuri ya Kiarabu ya Syria inatangaza kuwa inakubali mkataba wa usitishwaji mapigano," wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema Jumanne hii katika taarifa yake.

Nakala hii, hata hivyo, inabaini kwamba serikali itaendelea na "oparesheni za kijeshi katika mapambano dhidi ya ugaidi wa makundi ya Islamic State (IS), Al-Nosra Front na makundi mengine ya kigaidi ambayo yana uhusiano na makundi hayo mawili ya mwanzo kama ilivyotangazwa na Urusi pamoja na Marekani".

"Serikali ya Syria iko tayari kuratibu na upande wa Urusi ili kuamua maeneo na makundi ya waasi ambayo yatawajibika na mkataba huo wa usitishwaji mapigano," wizara ya Mambo ya Nje imeongeza.

Tangu kuanza kwa mgogoro nchini Syria mwaka 2011, uliosababisha watu zaidi ya 260,000 kuuwawa, serikali imekua haitofautishi kati ya wafuasi, waasi na wanajihadi, ikiwaita wote "magaidi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.