Pata taarifa kuu
Syria - Mzungumzo

Tume ya haki za Bindamu yalaumu kutumiwa kwa wananchi kama chambo katika mzozo wa Syria

Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa raia nchini Syria wanatumiwa kama chambo ya mazungumzo kufikia suluhu nchini humo pamoja na kutumia kama wapiganaji, suala ambalo tume hiyo inasema halikubaliki.

waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizungumza katika mkutano wa wafadhili wa Syria jijini London
waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizungumza katika mkutano wa wafadhili wa Syria jijini London Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake kwa wanahabari, mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja huo, Zeid Ra'aad Al Hussein alieleza hofu yake kuhusu kile alichokiita kuongezeka maradufu kuzorota kwa hali ya kibinadamu na kukithiri vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye mji wa Aleppo na maeneo jirani.

Msemaji wa ofisi hiyo, Cecile Pouyee amesema kuwa kumekuwa na matukio ya kushtua ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayotekelezwa kila siku nchini Syria.

Kwa upande wake Marekani kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje John Kerry, akiwa mjini Munich Ujerumani ambako amekutana na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, ameelezwa kufurahishwa na hatua waliyopiga kwenye mazungumzo yao kuelekea suluhu ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.