Pata taarifa kuu
YEMENI-MAPIGANO-USALAMA-SIASA

Yemen: mapigano yaendelea kurindima

Muungano wa Kiarabu unaopambana dhidi ya waasi wa Kishia nchini Yemen umetangaza Jumamosi hii kumalizika kwa muda wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano ulioanza kutekelezwa Desemba 15 lakini ulikua ukikiukwa kila mara tangu wakati huo.

Raia wa Yemen wakikagua kiwanda cha Coca-Cola kilioharibiwa na mashambulizi ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudia Arabia, jijini Sanaa Desemba 30, 2015.
Raia wa Yemen wakikagua kiwanda cha Coca-Cola kilioharibiwa na mashambulizi ya muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudia Arabia, jijini Sanaa Desemba 30, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kuna uwezekano kuwa mazungumzo huenda yakaanza upya katikati ya mwezi Januari.

Mkataba wa usitishwaji wa mapigano ulitangazwa na serikali ya Yemen ili kuashiria kuanza kwa mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja baina ya pande zinazopingana, mazungumzo ambayo yalifanyika Desemba 15 hadi 20 chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa nchini Uswisi.

Mkataba huo baadae uliongezwa, lakini mapigano, mashambulizi ya anga na urushwaji wa makombora viliendelea katika maeneo mengi nchini humo.

"Muungano wa Kiarabu kutoka jamii ya Wasuni umetangaza kumalizika kwa muda wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano nchini Yemen kuanzia saa 8:00 mchana" (Sawa na 5:00 mchana saa za kimataifa) Jumamosi hii", Tangazo rasmi limebaini. Tangazo hilo limewalaumu waasi, wakituhumiwa kutumia fursa ya mkataba huo kwa kuendelea kuyateka maeneo kadhaa.

Muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia uliingilia kati kijeshi nchini Yemen tangu mwezi Machi ili kuwafurusha waasi wa Kishia, wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na nchi ya Iran. Waasi wa Kishia wa Huthi waliiteka tangu mwishoni mwa mwaka 2014 sehemu kubwa ya nchi ya Yemen, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa Sanaa, ambapo serikali ya Yemen inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa ilitimuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.