Pata taarifa kuu
KUWAIT-YEMEN-USALAMA-USHIRIKIANO

Kuwait yaamua kupeleka askari Yemen

Kuwait imeamua kupeleka askari wa nchi kavu nchini Saudi Arabia kwa kushiriki katika vita nchini Yemen, ambako umoja wa Kiarabu ukiongozwa na Ryad unaendelea kupambana na waasi wa Kishia wa Huthi wanaoungwa mkono Iran, gazeti moja limearifu leo Jumanne.

Uharibifu uliosababishwa na shambulizi la anga katika mji wa Sanaa Oktoba 26, 2015.
Uharibifu uliosababishwa na shambulizi la anga katika mji wa Sanaa Oktoba 26, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ushiriki wa Kuwait katika vita nchini Yemen ulikua umejikita tu katika jeshi la anga.

Likinukuu chanzo kilio na taarifa sahihi, gazeti la Al-Qabas limearifu kwamba Baraza la mawaziri la Kuwaiti limepitisha uamzi wa kupelekwa wiki ijayo kwa askari nchini Saudi Arabia, ambapo watavuka mpaka na kuingia Yemen.

Muungano wa kijeshi wa Kiarabu uliingilia kati nchini Yemen mwishoni mwa mwezi Machi ili kuendesha mashambulizi ya anga, kisha operesheni za kijeshi za vya nchi kavu dhidi ya waasi wa Kishia wa Huthi na kuvisaidia vikosi vinavyoiunga mkono serikali inayotambuliwa kimataifa.

Licha Saudi Arabia na Kuwait, nchi nyingine za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Qatar, Misri na Sudan, wanashiriki katika muungano huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.