Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA-SIASA

Upinzani Syria wakubali kujadili, lakini Assad anatakiwa kuondoka

Makundi makuu ya upinzani nchini Syria yametangaza makubaliano yao Alhamisi katika mji wa Riyadh kwa mazungumzo na serikali ya Bashar al-Assad, lakini yametaka rais huyo aondoke madarakani kitakapoanza kipindi cha mpito.

Mawaziri wa nchi za Ghuba katika mji wa Riyadh Desemba 7, 2015 kabla ya mkutano kuhusu ya mgogoro wa Syria.
Mawaziri wa nchi za Ghuba katika mji wa Riyadh Desemba 7, 2015 kabla ya mkutano kuhusu ya mgogoro wa Syria. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Mkutano wa Riyadh, ambao umewaleta pamoja mamia ya wawakilishi wa upinzani wa kisiasa na jeshi, umelenga kuunganisha makundi hayo kwa ajili ya mazungumzo ili kumaliza mgogoro uliosababisha tangu mwaka 2011 vifo vya zaidi ya watu 250,000 na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.

Makubaliano haya yametangazwa siku moja kabla ya mkutano kuhusu Syria kati ya wawakilishi wa Urusi, Marekani na Umoja wa Mataifa mjini Geneva, wiki moja kabla ya mkutano mpya wa kimataifa mjini New York.

Katika taarifa uya mwisho iliyotolewa baada ya siku mbili za mazungumzo mjini Riyadh, washiriki walisema kuwa wako "tayari kuingia katika mazungumzo na wawakilishi wa serikali kwa misingi ya azimio la mkutano wa kwanza wGeneva (Juni 30, 2012) na maazimio husika ya kimataifa (...) katika kipindi watakachokubaliana na Umoja wa Mataifa."

Mkutano wa kwanza wa Geneva kati ya mataifa yenye nguvu ulieleza kipindi cha mpito nchini Syria, lakini giza limeendelea kutanda kuhusu hatima ya Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.