Pata taarifa kuu
SYRIA-MAPIGANO-USALAM

Watu elfu sabini waliuawa mwaka 2014 Syria

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema zaidi ya watu elfu 70 waliuawa katika mapigano yanayoendelea nchini Syria kati ya jeshi la serikali na makundi ya waasi mwaka 2014.

Kambi ya wakimbizi wa Syria katika mji wa Erbil, katika jimbo la Kikurdi la Iraq, Machi 29 mwaka 2014.
Kambi ya wakimbizi wa Syria katika mji wa Erbil, katika jimbo la Kikurdi la Iraq, Machi 29 mwaka 2014. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao wenye makao yao nchini Uingereza wanaochunguza mzozo wa Syria wamesema mwaka 2014 ulishuhudia mauaji makubwa katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na machafuko kwa mwaka wa nne sasa.

Inaelezwa kuwa mwaka uliopita, watu 17,790 waliouawa walikuwa raia wa kawaida huku 3,501 wakiwa watoto.

Rais Bashar Al Assad alionekana jana Alhamisi Januari 1 akiwa jijini Damascus akizungumza na wanajeshi wa serikali.

Wakati huo huo, watu 15,000 walipoteza maisha nchini Iraq mwaka jana, mauaji makubwa zaidi tangu mwaka 2007.

Mauaji mengi nchini Iraq yalisababishwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam ambalo linapambana na wanajeshi wa serikali kwa lengo la kutaka uongozi wa Kiislamu.

Nchini Iraq na Syria, muungano wa Mataifa 60 yanatumia mashambulizi ya angaa kupambana na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.