Pata taarifa kuu
SYRIA-WAASI-HOMS

Waasi wa Syria waondoka Homs bila hofu yoyote

Wapiganaji wa waasi na familia zao wameanza kuondoka asubuhi eneo la Homs, nchini Syria. Serikali ya Syria kwa upande wake, imejikubalisha kutowakamata wapiganaji hao na itawaruhusu kusafiri bila hofu yoyote, kaskazini mwa nchi hiyo, katika maeneo ambayo bado yanashikiliwa na waasi.

Zoezi la kuondoka kwa waasi wa Syria katika eneo laal-Waer katika mji wa Homs limeanza Jumatano Desemba 9, 2015.
Zoezi la kuondoka kwa waasi wa Syria katika eneo laal-Waer katika mji wa Homs limeanza Jumatano Desemba 9, 2015. REUTERS/Omar Sanadiki TPX IMAGES OF THE DA
Matangazo ya kibiashara

Ni mamia kadhaa ya watu, wapiganaji lakini pia raia wa kawaida, ambao wameaanza Jumatano hii asubuhi kuondoka katika kitongoji cha al-Waer eneo la mwisho ulililotekwa na waasi katika mji wa Homs. Kwa jumla, wapiganaji 2,000 wa waasi na familia zao watakua wameondoka katika eneo hilo mwishoni mwa wiki ijayo, kama yote yatakwenda kama ilivyopangwa.

Kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH), waasi hao wanapaswa kwenda kaskazini mwa Syria, katika mkoa wa Idleb, ambao bado unadhibitiwa na waasi.

Misaada ya kibinadamu

Makubaliano yaliosimamiwa na Umoja wa Mataifa yanasema kuwa waasi kabla ya kuondoka Homs, wanapaswa kurejesha silaha zao nzito nzito kwa mamlaka ya Syria. Zoezi la kubadilishana wafungwa pia limepangwa katika mchakato huo huo. Hatimaye, raia waliobaki katika eneo ambalo waasi wameondoka watakuwa na fursa ya kupata misaada ya kibinadamu, waliokua wakikosa tangu eneo hilo kuzingirwa kwa miezi kadha na wanajeshi wanaotii serikali ya Bashar Al Assad.

Pamoja na zoezi hili la kuondoka kwa waasi katika eneo la Homs ni ukurasa mpya unaofunuliwa, kwa sababu kitongoji cha al-Waer kilikuwa ni eneo la mwisho lililokua likidhibitiwa na waasi katika mji huo wa Homs - itakumbukwa mwaka 2014 makubaliano kama haya yalipelekea jeshi la Syria kupiga kambi upya katika mji wa zamani wa Homs.

Ushindi wa kishara kwa serikali

Mji wa Homs, baada ya mchakato kuondoka, utakuwa chini ya udhibiti kabisa wa utawala wa Bashar Assad. Serikali ya Syria kwa uhakika haitosita kufurahia ushindi wa kiishara, kwa sababu mji wa Homs kwa muda mrefu umekuwa kuonekana kama kitovu chamapinduzi ya Syria, na moja ya miji muhimu ya waasi. Homs hata hivyo iliwahi kupewa jina la mji mkuu wa mapinduzi, tangu kuanza kwa mgogoro wa Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.