Pata taarifa kuu
URUSI-SYRIA-IS-MASHAMBULIZI-USALAMA

Syria: Urusi imeanza mashambulizi dhidi ya IS

Manuari nne za kivita kutoka nchini Urusi zimeanza kutekeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.

helikopta ya kijeshi ya Urusi kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Latakia, Syria, Otoba 6, 2015..
helikopta ya kijeshi ya Urusi kwenye uwanja mdogo wa ndege wa Latakia, Syria, Otoba 6, 2015.. REUTERS/RURTR via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya yamethibitsihwa na rais Vladimir Putin na Waziri wa Ulinzi Sergei Shoigu.

Kiongozi huyo wa Urusi ameongeza kuwa jeshi lake litasiaidiana na lile la Syria kuhakikissha kuwa Islamic State wanaoondolewa katika ngome zao.

Aidha, Moscopw inasema ndege zakle za kivita zimerusha makombora yake na kulenga ngome 11 za wapiganaji hao.

Putin pia amesisitiza umuhimu wa nchi yake kushirikiana na Marekani, Uturuki na Saudi Arabia kufanikisha vita hivyo dhidi ya kundi la Islamic State.

Hata hivyo Marekani na Washirika wake wamekuwa wakikosoa namna Urusi inavyotekeleza mashmabulizi hayo na kuishtumu kuwalenga waasi wanaompinga Rais Bashar Al Assad.

Majeshi ya nchi za Magharibi NATO pia yameitaka Urusi kuachana na mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.