Pata taarifa kuu
SYRIA-URUSI-MAPIGANO-USALAMA

Assad apongeza mashambulizi ya Urusi Syria

Rais wa Syria Bashar Al Assad anasema hatua ya jeshi la Urusi kutekeleza mashambulizi ya anga dhidi ya makundi ya waasi na kundi la Islamic State katika nchi yake ni muhimu kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati.

Rais wa Syria Bashar Al Assad amesifu mashambulizi ya Urusi nchini mwake akibaini kwamba mashambulizi hayo ni muhimu kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati.
Rais wa Syria Bashar Al Assad amesifu mashambulizi ya Urusi nchini mwake akibaini kwamba mashambulizi hayo ni muhimu kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati. Reuters/Sana/Handout
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni nchini Iran, Rais Bashar Al Assad amesisitiza kuwa muungano wa jeshi kati ya Urusi, Iran na Iraq lazima ufanikiwe la sivyo eneo zima litaathiriwa.

Rais huyo wa Syria ameonyesha matumaini yake kuwa mashmabulzii yanayofanywa na Urusi yatasaidia kuleta utulivu nchini mwake.

Hata hivyo, hatua hii ya Urusi imeendelea kukukosolewa na mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani na kushtumu Urusi kuwalenga raia, tuhma ambazo Moscow inaendelea kukanusha.

Marekani na Uingereza zinataka juhudi zozote za kuleta amani nchini Syria zifanyike bila ya kumhusihsa Rais Assad lakini hili linapingwa na Urusi.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel naye amesema matumizi ya kijeshi peke yake hayatoshi kumaliza umwagaji damu nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.