Pata taarifa kuu
PALESTINA-GAZA-ISRAEL-VITA

Mwaka mmoja baada ya vita, raia wa Gaza wakata tamaa

Tarehe 8 Julai mwaka 2014, Israel iliendesha operesheni ijulikanayo kwa jina la " Eneo la Ulinzi " katika mji wa Gaza, nchini Palestina. Siku 50 za vita ambapo watu 2,200 upande wa Palestina, wengi wao wakiwa raia wa kawaida waliuawa. Upande wa Israel, watu 73, ikiwa ni pamoja na raia 6 wa kawaida waliuawa katika operesheni hiyo.

Chejaya, eneo lililo karibu na Gaza, ambalo ni moja ya maeneo yaliyoharibiwa katika vita.
Chejaya, eneo lililo karibu na Gaza, ambalo ni moja ya maeneo yaliyoharibiwa katika vita. .RFI/Murielle Paradon
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hiyo ilisababisha hasara kubwa. Nyumba 100,000 ziliteketezwa kabisa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Mwaka mmoja baadaye, ujenzi umekuwa vigumu kuanza, na raia wa Gaza wamekata tamaa.

Katika operesheni hiyo ambayo iligeuka kuwa vita, watu wengi walipoteza viungo vyao vya muili, hususaa katika mashambulizi ya angani ya Israel dhidi ya mji wa Jabaliya, Agosti 24 mwaka 2014.

“ Wakati huo nilikua na familia yangu katika bustani, baadae kulitokea mlipuko na sikumbuki kilichoendelea ”, amesema Thaer Juda, mmoja wa watu waliyonusurika katika vita hivyo, licha ya kupoteza kiungo chake cha mguu wakati nyumba yao ilishambuliwa kwa mabomu katika mji wa Jabaliya.

Hospitali za jimbo la Gaza zilikabiliwa wakati huo na uhaba wa dawa na vifaa vingine vya matibabu. Hata hivyo Thaer Juda alisafirishwa nchini Ujerumani kwa msaada wa shirika moja la kihisani. Alitibiwa kwa muda wa miezi kumi, na sasa anaweza kutembea akutumia mikono yake. Lakini hana tena matumaini. Mama yake na ndugu zake wanne waliuawa katika shambulio hilo.

Mashariki mwa jimbo la Gaza, katika mji wa Khuza, ujenzi wa nyumba zilizoteketezwa kwa mashambulizi ya angani ya Israel haujaanza. Barabara na nyumba viliharibiwa katika vita hivyo. Kwa sasa wakaazi wa mji huo wanakabiliwa na maisha duni.

Hatari ya kuewpo kwa misimamo mikali

Vijana hawana maisha ya baadae, kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya uchumi katika mji wa Gaza Omar Shaban.

" Theluthi mbili ya vijana hawajawahi kuondoka Gaza. Hawajasafiri kamwe. Hawana ajira. Hata hivyo walielimishwa, wanazungumza Kiingereza, wamekua wakiwasiliana na watu wengine kupitia mtandao wa Facebook. Wamekua wakilinganisha maisha yao na yale ya vijana Wazungu. Na tayari wameanza kuona tofauti, kubwa. Na hali hii inaweza kujenga misimamo mikali au kusababisha vita vipya ", amesema Omar Shaban.

Vijana hao huenda wakajiunga na makundi ya kiislamu yenye misimamo mikali kama Islamic State na Hamas ambayo yanaendesha mashambulizi ya hapa na pale katika maeneo mbalimbali nchini Israel na kungineko duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.