Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

Mkataba wa usitishwaji mapigano waanza kutekelezwa Jumane jioni

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen ambao wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa kigeni wakiongozwa na wale wa Saudi Arabia, wamekubali pendekezo la Saudi Arabia la kusitisha vita kwa siku tano.

Raia wakiendelea kuukimbia mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya kukumbwa na milipuko ya mabomu yanayorushwa na ndege za kivita za muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia.
Raia wakiendelea kuukimbia mji mkuu wa Yemen, Sanaa, baada ya kukumbwa na milipuko ya mabomu yanayorushwa na ndege za kivita za muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia. REUTERS/Mohamed al-Sayaghi
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wamechukua uamzi huo ili kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie watu wanaothiriwa na vita vinavyoendelea nchini Yemen.

Hata hivyo, Saudi Arabia imewaonya waasi hao kuwa itawashambulia ikiwa watavunja makubaliano hayo.

Hii inamaanisha kuwa vita vitasitishwa kuanzia leo Jumanne ili kutoa huduma hizo za kibiandamu ikiwemo misaada ya chakula na huduma za matibabu kwa waathiriwa.
Ni mwezi mmoja na nusu sasa tangu mapigano kati ya waasi wa kishia kutoka jamii ya Huthi na Muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kuendelea kushuhudiwa nchini Yemen.

Yemen ni nchi maskini ambayo inategemea chakula kutoka nje. Lakini pamoja na vita vinavyoendelea nchini humo, Saudi Arabia imeamuru bandari na barabara zote zifungwe.

Iran imekua ikilaumia kuwasaidia waasi wa Huthi. Shirika la Chakula Duniani (WFP) ilitangaza tarehe 30 Aprili kwamba linakabiliwa na uhaba wa mafuta ya gari na kubaini kwamba hali hiyo huenda ikawalazimu kusitisha kuendelea kutoa msaada wa chakula kwa raia wa Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.