Pata taarifa kuu
SAUDI ARABIA-YEMEN-VITA--SIASA

Wanajeshi watatu wa Saudi Arabia wauawa

Ni shambulio la kwanza dhidi ya Saudi Arabia. Saudi Arabia imethibitisha kuwa imewaua zaidi ya waasi wa Kishia kutoka Yemen kwenye mpaka wake na Saudi Arabia.

Mwanamgambo wa Yemen katika mji wa Aden wakati wa mapigano na waasi wa Huthi, Aprili 29 mwaka 2015.
Mwanamgambo wa Yemen katika mji wa Aden wakati wa mapigano na waasi wa Huthi, Aprili 29 mwaka 2015. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Kishia kutoka jamii ya Huthi wamekua wakisaidiwa na wanajeshi watiifu kwa rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh, kwa mujibu wa tangazo la shirika la habari la Saudi Arabia.

Tukio hilo limeelezwa " lisilo la kawaida ". Hii ni mara ya kwanza waasi wa kishia wakiendesha shambulio dhidi ya Saudi Arabia. Shambulio hilo lililoendeshwa na waasi wa kishia wakiungwa mkono na wanajeshi watiifu kwa rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh, ilikua likilenga kituo cha wanajeshi wa Saudi Arabia wanaotoa ulinzi kwenye mpaka wa Saudi Arabia na Yemen katika eneo la Najran, kusini mwa Saudi Arabia.

Wanajeshi watatu wa Saudi Arabia wameuawa katika kituo chao, lakini kwa mujibu wa shirika la habari la Saudi Arabia, waasi walirudishwa nyuma kwa msaada wa Jeshi la anga. Waasi tisa wa Kishia wameuawa, kulingana na tangazo lililotolewa na shirika hilo. Kwa upande wake wizara ya mambo ya ndani imetangaza kifo cha mwanajeshi, mlinzi wa mpaka wakati alipokua akipiga doria katika eneo jingine.

Saudi Arabia imeimarisha ulinzi nchi nzima. Vifaru, mizinga na silaha nzito za kivita na kamera vimewekwa kwenye mpaka wa Saudi Arabia na Yemen. Upande wa pili, nchini Yemen, wakaazi wa Aden wameendelea kushuhudia milipuko mikubwa tangu mwezi mmoja uliyopita. Milipuko ya mabomu na milio ya risasi vimekua vikisikika katika eneo moja karibu na uwanja wa ndege wa Aden. Mapigano kati ya wanamgambo wa Kishia na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yameendelea nchini Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.