Pata taarifa kuu
YEMEN-SAUDI ARABIA-HOUTHI-VITA-SIASA

Waasi wa Huthi wakubali kusitisha mapigano Yemen

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen ambao wamekuwa wakipambana na wanajeshi wa kigeni wakiongozwa na wale wa Saudi Arabia, wamekubali pendekezo la Saudi Arabia la kusitisha vita kwa siku tano.

Mtu huyu akijificha katika  kifusi vya nyumba yake katika mji wa Sanaa. Katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu chaa mapigano.
Mtu huyu akijificha katika kifusi vya nyumba yake katika mji wa Sanaa. Katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu chaa mapigano. REUTERS/Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wamechukua uamzi huo ili kuruhusu misaada ya kibinadamu iwafikie watu wanaothiriwa na vita vinavyoendelea nchini Yemen.

Hata hivyo, Saudi Arabia imewaonya waasi hao kuwa itawashambulia ikiwa watavunja makubaliano hayo.

Hii inamaanisha kuwa vita vitasitishwa kuanzia siku ya Jumanne wiki hii ili kutoa huduma hizo za kibiandamu ikiwemo misaada ya chakula na huduma za matibabu kwa waathiriwa.

Ni mwezi mmoja na nusu sasa tangu mapigano kati ya waasi wa kishia kutoka jamii ya Huthi na Muungano wa nchi za kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia kuendelea kushuhudiwa nchini Yemen.

Yemen ni nchi maskini ambayo inategemea chakula kutoka nje. Lakini pamoja na vita vinavyoendelea nchini humo, Saudi Arabia imeamuru bandari na barabara zote zifungwe.

Iran imekua ikilaumia kuwasaidia waasi wa Huthi. Shirika la Chakula Duniani (WFP) ilitangaza tarehe 30 Aprili kwamba linakabiliwa na uhaba wa mafuta ya gari na kubaini kwamba hali hiyo huenda ikawalazimu kusitisha kuendelea kutoa msaada wa chakula kwa raia wa Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.