Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS-Usalama

Hali ya taharuki yaendelea kutanda Isreli na Palestina

Ijumaa hii ni siku inayoandaliwa swala kubwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, wakati wapalestina wanaomboleza kifo cha kijana mwenye umri wa miaka 17, alieuawa katika mazingira ya ulipizaji kisase, baada ya vijana 3 wa kiisraeli kuokotwa maiti. Muili wa kijana huyo wa kipalestina unatazamiwa kuzikwa ijumaa hii, baada ya swala ya Ijumaa.

hali ya wasiwasi yaendelea kutanda Isreli na Plaestina kufuatia hofu ya kutokea machafuko.
hali ya wasiwasi yaendelea kutanda Isreli na Plaestina kufuatia hofu ya kutokea machafuko. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Kunasubiriwa mamia kwa maelfu ya waumini wa kiislamu kwenye msikiti wa Jerusalem. Polisi imeimarisha ulinzi na usalama pembezuni mwa mji huyo wa zamani ili kukinga machafuko ambayo yanaweza kutokea kwa wakati wowote baada ya swla ya Ijumaa. Hali ya taharuki imetanda hivi karibuni kufutia kifo cha kijana huyo wa kipalestina, Mohamed Abou Khdeir, alietekwa nyara na kuuawa Jumatano wiki hii, katika mazingira yanayosadikiwa kuwa ni ya ulipizaji kisase baada ya vijana watatu wa kiisreli kuokotwa maiti.

“Familia ya Abou Khdeir imeweka hema mbele ya nyumba yao kwa ajili ya msiba. Na mazishi yatafanyika baada ya swala ya Ijumaa”, baba wa marehemu amethibitsha, huku akibaini kwamba mazishi ya kijana wao yalicheleweshwa kutokana na vipimo walivyokua wakifanyia maiti. Kwa mujibu wa mama wa marehemu, waisraeli walikua wameomba pia mazishi yafanyiwe kwa siri, hususan usiku ili kuepusha machafuko, lakini makubaliano yameafikiwa, amethibitisha mama huyo.

Familia na wakaazi wa mji wa Shuafat wamepandwa na hasira, Wanabaini kwamba poilsi haikuingilia mapema ili kijana huyo wakipalestina asitekwi nyara na kuuawa. Raia hao wameinyooshea kidole polisi kwamba haijafanya chochote ili kuwafichua wahalifu. Wamebaini kwamba polisi ilipewa taarifa mapema hata camera zilirikodi tukio hilo la kutekwa nyara kwa kijana huyo, wamezidi kusema raia hao. Kumekua hivi karibuni na majaribio ya utekaji nyara katika mji huyo.

Katika ukanda wa gaza, hali ya wasiwasi imetanda. Baraza la kitaifa la usalama la Israeli lilikutana alhamisi wiki hii ili kujadili kuhusu hali ya usalama kwenye mpaka na Palestina. Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Isreli, nchi yake inajiandaa kwa mambo mawili : Iwapo kitendo cha wapalestina cha kurusha makombora kusini mwa Israeli kitasitishwa, amani itapatikana. Kinyume cha hivo, jeshi la Israeli litaendelea na harakati zake, amesema Benjamin Netanyahu.

Kwa upande wake, mkuu wa majeshi ya Israeli, jenerali Benny Gantz, ametahadharisha kupitia akaunti yake ya Twitter : “ Tunataka amani, lakini endapo Hamas itaendesha mashambulizi dhidi yetu, basi hatutosita kujibu”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.