Pata taarifa kuu
ISRAELI-HAMAS-Usalama

Hali ya taharuki yatanda kati ya Israeli na Hamas

Vijana watatu wa kiisraeli waliotekwa nyara Juni 12 wameokotwa maiti kusini mwa mwa eneo linaloshikiliwa la Cisjodanie. Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema vijana hao waliuawa kikatili.

Picha za wanafunzi 3 wa kkisrael ambazo ziliunganishwa , Naftali Fraenkel miaka 16 (kushoto), , Gil-Ad Shaer, miaka 16 (katikati), na Eyal Yifrah, miaka 19 (kulia).
Picha za wanafunzi 3 wa kkisrael ambazo ziliunganishwa , Naftali Fraenkel miaka 16 (kushoto), , Gil-Ad Shaer, miaka 16 (katikati), na Eyal Yifrah, miaka 19 (kulia). REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Netanyahu amelinyooshea kidole cha lawama kundi la Hamas na kuahidi kulipiza kisase.

Vijana hao, Eyal Yifrach mwenye umri wa miaka 19, Naftali Frankel na Gilag Shaer ambao wote wawili walikua na umri wa miaka 16 walikua wanafunzi katika chuo cha kidini katika maeneo ya walowezi wa kiyahudi. Wote hao watatu waliokotwa maiti ando na kijiji cha Halhoul, karibu na barabara walikoonekana mara ya mwisho.

“Miili ya vijana hao iligunduliwa na jeshi katika eneo lilioko kaskazini magharibi ya wilaya ya Hebron”, msemaji wa jeshi la Israeli Peter Lerner amewathibitishia wanahabari.

Miili hio ilisafirishwa ili ifanyiwe vipimo vya uchunguzi kwa lengo la kuwatambua na kuchunguza tarehe waliyouawa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Israeli, vijana hao waliuawa baada ya kutekwa nyara.

“Walitekwa nyara na baadae kuuawa kikatili na wanyama wanaofanana na binadamu”, amesema Netanyahu, huku akibaini kwamba kundi la Hamas linahusika na vifo vya vijana hao. Waziri huyo mkuu wa Israeli ameahidi kulipiza kisase kwa kundi la Hamas

Kwa upande wake Hamas imekana katu katu kuhusika na mauaji hayo, na imeapa kujihami iwapo itashambuliwa. Awali Hamas ilipongeza kutekwa nyara kwa vijana hao.

“Iwapo walowezi wataanzisha mashambulizi au vita dhidi yetu, watakua wamekaribisha vita visiyo kuwa na kikomo”, amesema msemaji wa kundi la Hamas, Sami Abu Zuhri.

Hayo yakijiri jeshi la anga la Israeli limeshambulia usiku wa jana kuamkia leo ukanda wa Gaza, bila hata hivo kusababisha hasara, wanahabari wa shirikas la habari la AFP wamethibitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.