UKWELI AU UONGO
Labenevolencija na RFI Kiswahili watoa mafunzo ya habari za kupotosha mitandaoni
Imechapishwa:
Cheza - 10:00
Picha inayosambaa mtandaoni ya Moïse Katumbi na rais wa Kenya, William Ruto ikidai kuwa ina uhusiano na kuundwa kwa vuguvugu la Corneille Nangaa wa AFC inapotosha umma.
Matangazo ya kibiashara
Picha hii ni ya Disemba 18, 2022 na kipindi ambacho Katumbi anadaiwa kuwa nchini Kenya mwaka huu, alikuwa kwenye kampeni za uchaguzi huko Lualaba nchini DRC.
Utasikiliza pia baadhi ya maoni ya waliohudhuria mafunzo kuhusu habari za ukweli au uongo kutoka kule Bukavu nchini DRC na pia kule Kigali nchini Rwanda mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu.