UKWELI AU UONGO
Zambia: Video ya kupotosha kuwa rais Hichilema ametangaza kutowania tena urais
Imechapishwa:
Cheza - 10:00
Hivi leo moja ya habari tunayoangazia ni video iliundwa kwa kutumia akili mnemba ikionyesha rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametangaza kutowania urais katika uchaguzi ujao.
Matangazo ya kibiashara
Huu ni uongo, video hii imeundwa kidijitali kwa kutumia akili mnemba yaani Artificial Intelligence. Katika video hii msikilizaji, rais Hichilema anaonekana kuvalia suti ya buluu iliyokoza na tai nyekundu, nyuma yake bendera ya nchi yake inaonekana.