Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Barabara nchini Ujerumani imepewa jina la Eliud Kipchoge: Sio kweli

Imechapishwa:

Mwanariadha Eliud Kipchoge kutoka Kenya mara kwa mara ameweka rekodi duniani ya kuwa mwanariadha bora na kwa mara ya tano hivi maajuzi Septesmba 24, alishinda mbio za Berlin Marathon kwa mara ya tano.

Madai ya kupotosha kuwa barabara moja nchini Ujerumani ilipewa jina la Eliud Kipchoge kutoka Kenya
Madai ya kupotosha kuwa barabara moja nchini Ujerumani ilipewa jina la Eliud Kipchoge kutoka Kenya © FMM
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ushindi wake ulioshabikiwa sana, machapisho yaliibuka mitandaoni yakiwa na picha ya bango la barabarani katika mji mkuu wa Ujerumani linalodaiwa kuwa na jina la Kipchoge. Baadhi walidai Mkenya huyo alikuwa akituzwa kwa ushujaa wake.

Lakini dai hili la Septemba 24 linapotosha. Waandishi wa habari wa shirika la AFP huko Berlin walithibitisha madai haya ni ya kupotosha. Pia maofisa wa mji huo walikanusha hilo.

Madai haya yalisambazwa baada ya Kipchoge kushinda mbio za Berlin kwa mara ya tano kwa kutumia saa 2, dakika 2 na sekunde 42. Na siku chache kabla ya mbio hizo, mchoro wa bingwa huyu wa Olimpiki ulizinduliwa huko Berlin.

Mchoro huu wa Kipchoge kabla ya kuanza kwa mbio hizo uliangaziwa katika ripoti nchini Kenya ikiwemo kwenye gazeti la the Star na pia Daily Nation. Lakini madai ya barabara hiyo kupewa jina la Kipchoge ni ya kupotosha.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.