Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Sauti feki ya rais Macron kuhusu maandamano mjini Goma DRC

Imechapishwa:

Tunaangazia video iliyokuwa na sauti feki ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu maandamano ya Goma nchini DRC.

Tunaangazia video iliyokuwa na sauti feki ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu maandamano ya Goma nchini DRC.
Tunaangazia video iliyokuwa na sauti feki ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu maandamano ya Goma nchini DRC. © FMM
Matangazo ya kibiashara

Takriban wiki mbili zilizopita, maandamano dhidi ya MONUSCO yalifanyika haswa eneo la Goma nchini DRC ambapo watu waliuawa.

Kwa sasa wanajeshi sita wakiwemo maafisa wakuu wawili wako mbele ya mahakama kutokana na mauaji hayo.

Lakini sasa msikilizaji kuna video iliyoenea sana kwenye makundi ya whatsapp na Tiktok hata sisi katika kitengo hiki tuliipata, ikiwa na madai ya uongo. Ilikuwa na swali lililosema hivi, “Je! Emmanuel Macron anaweza kuwa alijibu ukandamizaji mbaya wa maandamano huko Goma mnamo Agosti 30, 2023, katika mahojiano na France 24?

Katika video hii, tunasikia sauti, inayowasilishwa kama ya rais Macron, juu ya picha za wanajeshi wa Kongo wakirundika maiti kwenye lori. Sauti inasikika ikimshambulia rais wa zamani Kabila, kisha Félix Tshisekedi na chama chake, UDPS:

Ukweli ni kuwa, Emmanuel Macron hakuwahi kutoa matamshi haya, wala kwenye France 24, kama vile nembo iliyobandikwa kwenye video hii inajaribu kukufanya uamini, wala kwingineko.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.