UKWELI AU UONGO
Video inayosambazwa ikielezwa ni wanajeshi wa Nigeria wakiingia Niger: Ni uongo
Imechapishwa:
Cheza - 10:00
Siku kadhaa baada ya ECOWAS kutangaza kukubaliana kuhusu makataa ya kutuma vikosi vya usalama nchini Niger, video imesambazwa mtandaoni ikiwa na madai ya kuonesha ni wanajeshi wa Nigeria wakiingia Niamey.
Matangazo ya kibiashara
Lakini madai haya ni ya uongo. Video hii ni ya ripoti ya shirika la habari la CNN kuhusu mgogoro wa kibinadamu wa hivi karibuni katika eneo la Darfur kule Sudan, ambayo ilichapishwa Julai 21, raia wakikimbilia nchi ya Chad.