Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Ubalozi wa Ufaransa nchini Niger haukuteketezwa moto kama inavyodaiwa

Imechapishwa:

Nchini Niger kuna video  za kupotosha zikioonyesha ubalozi wa Ufaransa jijini Niamey, ukiwa umeporwa kabisa na kuharibiwa.

Taarifa za kupotosha kwamba ubalozi wa Ufaransa nchini Niger uliharibiwa vibaya na kuchomwa moto na waandamanaji
Taarifa za kupotosha kwamba ubalozi wa Ufaransa nchini Niger uliharibiwa vibaya na kuchomwa moto na waandamanaji © FMM
Matangazo ya kibiashara

Video hii inapotosha. Mnamo Julai 30, shirika la habari la AP, lilichapisha picha na video ya matukio nchini Niger.

Shirika la AP liliendelea kusema, lango la ubalozi huo liliteketezwa moto huku maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono mapinduzi wakiaandamana katika mitaa ya mji mkuu, Niamey.

Shambulio hili lilikuja siku moja baada ya Ufaransa kufuta msaada wa maendeleo na kifedha kwa Niger baada ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais Mohamed Bazoum.

Shirika la CNN Julai 31, katika moja ya taarifa zake iliandika, “vikosi vya usalama vya Nigeria walitumia gesi za kutoa machozi katika jaribio la kuwatawanya waandamanaji. Moja ya picha kutoka eneo la tukio ilionyesha watu wakijaribu kuanzisha moto nje ya ua.

Pia tarehe mosi mwezi huu, CBC News pia iliandika

“Video kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha waandamanaji wakijaribu kuvunja mlango wa ubalozi huo.

Tunaweza kuthibitisha kuwa ndio kulikuwa na shambulio katika lango la ubalozi wa Ufaransa lakini vídeo inayoonyesha êneo fulani likiharibiwa na kuporwa sio jengo la ubalozi huo huko Niamey.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.