Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Waziri wa fedha wa Niger alilia akitakiwa kueleza kuhusu pesa zilizopotea: Uongo

Imechapishwa:

Nchini Niger kumefanyika mapinduzi lakini habari za kupotosha zimekuwa nyingi katika mitandao ya kijamii ambapo sasa kuna hii video inayodai waziri wa fedha wa Niger katika serikali Mohamed Bazoum iliyooangsuhwa akilia baada ya wanajeshi kumtaka aeleze kuhusu pesa zilizopotea.

Video inayodai waziri wa fedha wa Niger katika serikali Mohamed Bazoum iliyooangsuhwa akilia baada ya wanajeshi kumtaka aeleze kuhusu pesa zilizopotea
Video inayodai waziri wa fedha wa Niger katika serikali Mohamed Bazoum iliyooangsuhwa akilia baada ya wanajeshi kumtaka aeleze kuhusu pesa zilizopotea © FMM
Matangazo ya kibiashara

Kinyume na ilivyo, video hii ni ya Disemba mwaka 2021, na inamuonyesha aliyekuwa Waziri wa Sheria wa Niger Marou Amadou akilia baada ya kutoa heshima kwa rais wake wa zamani.

Msikilizaji ukiitafuta asili ya video hii, utapata ilichapishwa kwenye mtandao wa facebook mnamo Disemba 28, 2021. Kichwa chake kinasoma hivi

 “Marou Amadou bani? Je, ni heshima kwa rais wa zamani inayokufanya ulie?

Walakini, picha za mkutano huo zinalingana na video iliyoenea. Marou Amadou amevalia vazi lile lile la samawati, saa ile ile, skafu ya kijani kibichi, na anasimama mbele ya kipaza sauti cheusi, akiwa ameketi kwenye kiti.

Kulingana na ukurasa wa ucheshi wa Niger Niamey Délire, Marou Amadou alilia baada ya kumshukuru Mahamadou Issoufou kwa kumkabidhi wizara ya Sheria kwa miaka 10, habari ambayo ilithibitishwa na mwandishi wa habari wa nchi hiyo aliyewasiliana na wahariri wa makala ya The Observers kwenye runinga ya France 24 ambao tunashirikiana katika kazi hii.

Basi ndipo kwenye kipindi hiki tunathibitisha kuwa video hii haimwonyeshi waziri wa fedha wa Niger akilia baada ya kutishiwa na jeshi bali ni video ya waziri wa zamani wa sheria akimuomboleza rais wa zamani wa niger mwaka 2021.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.