Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Urusi imekuwa ikitumia propaganda dhidi ya mataifa magharibi barani Afrika

Imechapishwa:

Nchi ya Ufaransa kwa miaka mingi imekuwa ikiibua madai ya Urusi kueneza propaganda haswa katika mataifa ambayo kundi la Wagner linahudumu haswa Afrika. Ufaransa imeituhumu Urusi kwa kuiga tovuti za vyombo vya habari vya Ufaransa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, kwa lengo la kueneza mkanganyiko na taarifa za uongo kuhusu vita vya Ukraine.

Urusi imekuwa ikiendeleza taarifa za kupotosha barani Afrika dhidi ya Ufaransa na mataifa ya Magharibi
Urusi imekuwa ikiendeleza taarifa za kupotosha barani Afrika dhidi ya Ufaransa na mataifa ya Magharibi © fmm
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Februari, Umoja wa Ulaya ulitangaza vikwazo kwa kundi hili kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na kueneza propaganda haswa Afrika. Ikumbukwe Urusi na Wagner wana rekodi ya kupotosha umma kupitia vyombo vya habari na nakumbuka mkuu wake Yevgeny Prighozin alikiri kuhusika na suala hili.

Tangu Urusi ivamie Ukraine, wandani wa Urusi wameeneza propaganda mitandaoni na nadharia za njama, kwa lengo la kufanya uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa kwa Ukraine kufifia, na umekuwa ni kama mchezo wa paka na nyama maana kila mara utawala wa Kremlin hubadilisha mbinu wanayotumia.

Kwa mfano, kuna hivi maajuzi kulikuwa na maandamano nchini Ufaransa baada ya kijana mwenye umri wa miaka 17 kuuawa na polisi.

Ndio, maandamano hayo yalifanyika na yaligeuka kuwa ya ghasia, lakini video zinazosambaa mtandaoni zimechanganywa na video za zamani wakati wa maandamano dhidi ya umri wa kustaafu.

Kitu ambacho utagundua ni kuwa video hizi zinasambazwa nchini DRC, nchi ambayo Urusi iko mbioni kushawishi na hashtag iliyo kwenye video hizi inaeleza wazi  kwamba zimedhaminiwa.

Msikilizaji, hatutaki uegemee upande wowote kuhusu hili, lakini ni jukumu letu kukufanya uelewe jinsi habari za uongo na za kupotosha zimekuwa zikiongezeka.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.