Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

MOUNSCO inashawishi kuachiwa kwa kanali wa RDF anayezuiliwa DRC: Sio Kweli

Imechapishwa:

Kuna taarifa ambayo imekuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii haswa mashariki mwa DRC, ikiwa na madai kuwa MONUSCO inajaribu kuwashawishi wapiganaji waasi ili wamuachie mtu aliyetajwa kwa jina la kanali Ngendahimana, wa kitengo cha RDF, ambaye anazuiliwa huko Rutshuru.https://www.facebook.com/photo?fbid=217581297806300&set=a.111942018370229

Taarifa za kupotosha kuwa MONUSCO inashawisha kuachiwa huru kwa afisa wa jeshi wa Rwanda anayezuiliwa nchini DRC
Taarifa za kupotosha kuwa MONUSCO inashawisha kuachiwa huru kwa afisa wa jeshi wa Rwanda anayezuiliwa nchini DRC Β© FMM
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huu uliambatana na picha inayoonyesha kile kinachooneka kuwa wanajeshi, baadhi yao wakiwa wamevalia sare za Umoja wa Mataifa, na nyuma yake tunaona lori la Umoja huo.

Na kwa sababu picha hii inaonekana kupigwa kutoka kwenye eneo la kijeshi, tulitaka kujua pahali picha asili ipo kwa sababu picha hii tuliyoona haikuwa kamilifu, inaoneka kwamba baadhi ya maelezo yameondolewa.

Utafiti wetu unatupeleka kwa picha iliyochapishwa Februari 23, mwaka huu katika ukurasa wa MONUSCO, ikiwa na kichwa Beni: MONUSCO yafunga kambi yake ya kijeshi huko Mutwanga. Hapa picha ina maelezo yote na haijakarabatiwa kama ile iliyokuwa ikisambaa kwenye makundi ya kijamii.

https://peacekeeping.un.org/en/beni-monusco-shuts-its-military-base-mutwanga

Katika picha hii asili, mtu ambaye alikuwa ameondolewa kwenye picha hiyo kupitia ukarabati, anaonekana na malori ya Umoja wa Mataifa yanaonekana pia.

Tulifanya uchunguzi zaidi na kwenye akaunti rasmi ya twitter ya MONUSCO, tulipata kuwa habari hii ilikuwa imetangazwa kuwa feki.

https://twitter.com/MONUSCO/status/1667733146853416960

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.