Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Kenya: Paul Mackenzie ni mwanachama wa chama cha ODM chake Odinga: Uongo

Imechapishwa:

Kuna madai kwenye makundi ya mitandao ya kijamii nchini Kenya kuwa Paul Mackenzie -huyu ni mhubiri tata anayetuhumiwa kuwachochea wafuasi wake kufunga kula hadi kufa- kuwa yeye ni mwanachama wa chama cha ODM, kupitia chapisho la Aprili 26 mwaka huu kwenye mtandao wa facebook.

Picha za kupotosha kuwa Paul Mackenzie ni mwanachama wa ODM
Picha za kupotosha kuwa Paul Mackenzie ni mwanachama wa ODM © FMM
Matangazo ya kibiashara

Chapisho lilisoma hivi na nanukuu "Mackenzie anamwamini Mungu wa kweli aliye hai, kwa nini anamtaka kiongozi wa AZIMIO Raila Odinga kuingilia kati na kumnusuru na kile anachokiita 'mateso ya kisiasa' kutokana na uhusiano wake naye? Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, aliyasema hayo akiwa mahakamani?"

Pïcha hiyo hiyo ilichapishwa na mtumizi mwingine wa facebook ikisema: Pasta Mackenzie ni mwanachama wa ODM, Raila muokoe. Chapisho hilo pia lilsambazwa tena na kundi linaloitwa Statehouse Kenya Forum, na pia kusamabzwa kwenye twitter.

Uchunguzi wetu tumegundua kuwa picha hii ilibadilishwa kuashiria uhusiano kati ya Mackenzie and Odinga. Utafiti tuliofanya kwa kutumia, reverse image search, ilionyesha picha hiyo kwenye ripoti iliyochapishwa nchini humo kwenye toleo la Nairobi News, inayoonyesha fulana ya chungwa ya Mackenzie ikiwa na nembo ya kituo chake cha televisheni cha Times TV.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.