Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

DRC: Taarifa za kupotosha kwamba MONSUCO ilimsafirisha Makanika kukutana na EAC Bunagana

Imechapishwa:

Wiki hii tunaangazia picha ambayo imekuwa ikisambazwa katika mitandao ya kijamii haswa twitter na facebook nchini DRC haswa katika eneo la mashariki. 

Taarifa za kupotosha kuwa tume ya walinda amani wa umoja mataifa nchini DRC MONUSCO, ilimsafirisha mtu anayedaiwa kuwa muasi kukutana na EAC
Taarifa za kupotosha kuwa tume ya walinda amani wa umoja mataifa nchini DRC MONUSCO, ilimsafirisha mtu anayedaiwa kuwa muasi kukutana na EAC © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwenye picha hii, wanaume watatu wanaonekana wakiwa wamevalia sare za kijeshi katika eneo linalodaiwa kuwa Bunagana nchini DRC. 

Kando na hii picha, kuna maelezo marefu tu yamechapishwa. Sasa hapa msikilizaji uwe makini maana tunaenda kupeleka hatua kwa hatua iliuelewe nini tunachokizungumzia kuhusu picha hii ambayo nasi wenyewe tumebaini ni ya kupotosha. 

Taarifa hii ilichapishwa Jumanne ya tarehe 18 ya mwezi huu katika lugha ya kifaransa kwenye mtandao wa facebook kwa kutumia akaunti kwa jina la L'opération de l'auto-défense Maï-Maï kabla ya kusambazwa katika makundi mengine nchini DRC ikiwemo, Congo wazalendo. 

Kumbuka hapo mwanzoni tumesema kuwa taarifa hii ilidai kwamba tume ya walinda amani wa umoja wa mataifa nchini DRC MONUSCO, ilihusika na kumsafirisha Makanika kukutana na EAC –Tulitaka kujuwa kutoka kwa uongozi wa tume hiyo iwapo ni kweli walihusika moja kwa moja au mfanyikazi wao alihusika. 

Tumempigia msemaji wa mkuu wa MONUSCO nchini DRC Bintou Keita, Khady lo Porte-Parole ambaye alikana kuhusika na madai haya.

Vile vile EAC nayo pia ilikana kuhusika na kwamba taarifa hii ilikuwa ya uongo.

Vipindi vingine
  • 10:18
  • 10:00
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.