Pata taarifa kuu
UKWELI AU UONGO

Kenya: Odinga alilazwa baada ya maandamano ya mwezi Machi: Uongo

Imechapishwa:

Nchini Kenya picha ya zamani imeanza tena kusambaa ikimuonyesha Raila Odinga, waziri mkuu wa zamani nchini humo akihudumiwa na madaktari, picha hii ikidai kuwa Odinga alianza kulalamikia maumivu ya kifua baada ya maandamano aliyoongoza jijini Nairobi mwezi Machi mwaka huu.

Habari za kupotosha kuwa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, alilazwa baada ya maandamano ya Machi, 2023
Habari za kupotosha kuwa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, alilazwa baada ya maandamano ya Machi, 2023 © FMM
Matangazo ya kibiashara

Sasa hapa, picha ni ya Odinga ndio, tatizo ni kwamba tukio lilifanyika mwaka wa 2017 wakati kiongozi huyo alipolazwa hospitalini kwa kile kilichodhaniwa kuwa alikula chakula chenye sumu yaani alikuwa na food poisoning.

Muungano wa Azimio la Umoja wake Odinga umethibitisha kuwa mwanasiasa huyo mkongwe hakuwa mgonjwa wakati wa mikutano ya hadhara ya hivi karibuni.

Uchunguzi ambao tumeufanya kuhusu picha hii ambao pia ulifanywa na AFP umebaini kuwa picha hii ilichapishwa zaidi ya miaka mitano iliyopita, wakati huo Odinga alikuwa akiwania urais kwa tiketi ya National Super Alliance (NASA) dhidi ya rais wa zamani Uhuru Kenyatta na wala sio kama inavyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa pciha hii ni ya mwezi jana.

Vipindi vingine
  • 10:00
  • 10:58
  • 10:01
  • 10:01
  • 10:01
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.