Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Jamii katika Pwani ya Kenya inavyotumia mswaki "Toothbrush" kurejesha mifumoikilojia ya matumbawe
Mkutano wa mazingira wa kimataifa COP28 unaendelea jijini Dubai, Saudi Arabia, lengo lake likiwa ni kuangazia namna ya dunia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.07/12/202310:00 -
Mikoko: Wanawake Lamu mbioni kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa
Athari za mabadiliko ya hali ya hewa hazichagui mtoto au mtu mzima, akina mama wamelichukua kuwa jukumu lao kuhakikisha mikakati imefanikishwa katika harakati za kupunguza athari hizi haswa kupitia upanzi na uhifadhi wa mikoko27/11/202310:00 -
Maendeleo kidogo katika mazungumzo ya mkataba wa kukomesha uchafuzi wa plastiki
Msikilizaji kwa juma moja, wajumbe kutoka mataifa takriban 175, walikusanyika jijini Nairobi kwa majadiliano ya awamu ya tatu kuelekea kuundwa kwa mkataba wa kisheria wa kimataifa kupambana na uchafuzi utokanao na taka za plasitki ikiwa ni pamoja na mazingira ya baharini.Katika kipindi hiki, wajumbe wa serikali na wadau wengine kutoka mashirika yasio ya kiserikali walikuwa wakijadili mapendekeo ya maudhui yanayofaa kujumuishwa kwenye mkataba huo wa kisheria.21/11/202310:00 -
Namna mabadiliko ya tabianchi inavyozidisha mahitaji ya kibinadamu katika nchi tofauti duniani
14/11/202310:00 -
09:55
-
Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania, maarufu EACOP
Makala ya mazingira lezo dunia yako kesho juma hili, yanaangazia mradi huu wa ujenzi wa bomba la kusafirishia mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanzania, maarufu kama EACOP, mradi ambao unatazamiwa kugharimu dola bilioni 5.24/10/202309:34 -
Jamii ya Endorois nchini Kenya yaendelea kutaabika kutokana na kupanda kwa kina cha ziwa Bogoria
Kulingana na ripoti ya wataalam, maziwa yanayopatikana eneo la Afrika mashariki yameendelelea kurekodi ongezeko ya kasi ya viwango vya maji, hali inayotajwa kuchangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Nchini Kenya hali hii imeendelea kushuhudiwa kwenye maziwa yanayopatikana katika eneo la bonde la ufa.16/10/202310:00 -
Utayari na mikakati ya nchi za Afrika Mashariki kudhibiti majanga katika kipindi cha El Nino
Kulingana na wataalam, hali ya mabadiliko ya tabianchi imechangia pakubwa matukio ya el nino ambayo kwakawaida, athari zake hazitabiriki, lakini huathiri hali ya hewa duniani, kuanzia joto kali, mvua nyingi huku pia ikisababisha hali ya ukame katika baadhiya maeneo04/10/202309:30 -
Athari ya sekta ya nguo kwenye mazingira, inachangia asilimia 8 ya utoaji wa gesi joto duniani
Kulingna na UNEP, sekta hiyo inachangia asilimia 8 ya utoaji wa gesi joto duniani ambayo inachangia mabadiliko ya tabianchi.Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la mazingira la Greenpeace, vitambaa vinavyotumiwa kutengeneza nguo ni nyuzi za sanisia ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye mafuta ya kisukuku ambayo pia ni hatari kwa mazingira22/09/202310:00 -
Matumizi ya magari na pikipiki za umeme nchini Kenya katika kupunguza uchafuzi wa hewa
Kenya iko mbioni kuimairisha sekta ya usafiri wa uma, na kampuni ya kutengeneza magari ya Roam ni miongoni mwa zinazolenga kutumia fursa hiyo kuchangia katika kupunguza uchafuzi wa hewa unaotokanana sekta ya usafiri.11/09/202310:00 -
Azimio la kongamano la Afrika kuhusu tabianchi, ukosoaji kutoka kwa wanaharakati wa mazingira
Mkutano wa tabianchi jijini Nairobi, ulikusudiwa kuja na azimio la pamoja kuhusu msimamo wa bara hilo kuhusu kukailiana na mabadiliko ya tabianchi. Ahadi ya Dola Bilioni 23 iliahidiwa na wadau kutoka mataifa mbalimbali, kusaidia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, barani Afrika.11/09/202310:00 -
Shirika la PELUM Kenya laandaa hafla ya vijana kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana
Vijana zaidi ya 20 walipata fursa ya kujifunza kutoka kikundi cha wazee cha Va-Mweki kutoka eneo la Kivaa, kaunti ya Machakos, nchini Kenya, kuhusu utunzaji wa mazingira kwa kutumia njia ya kitamaduni na uhifadhi wa tamaduni za jamii ya wakamba inayopatikana nchini Kenya.28/08/202310:00 -
Matarajio ya wadau wa mazingira kuhusu kongamano la mazingira la Afrika
Kongamano la mazingira la Afrika litaandaliwa jijini Nairobi nchini Kenya kuanzia Septemba 4-6 2023.28/08/202309:57 -
Uchimba madini na changamoto za utunzwaji wa mazingira
Kulingana na shirika la mazingira la Umoja wa mataifa, UNEP, kuna wachimba madini karibu milioni 20 katika nchi zaidi ya 80, idadi hii ikijumuisha wambimba madidi wadogowadogo,Nchini kenya, mchakato wa kupata madini ya dhahabu huwa ni ngumu sana. Mwenzangu George Ajowi alizuri eneo la Osiri kaunti ya Migori magahribi mwa kenya, na kushuhudia jinsi dhahabu hutafutwa usiku na mchana.22/08/202310:01 -
09:59
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.