Pata taarifa kuu
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Mikoko: Wanawake Lamu mbioni kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Imechapishwa:

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa hazichagui mtoto au mtu mzima, akina mama wamelichukua kuwa jukumu lao kuhakikisha mikakati imefanikishwa katika harakati za kupunguza athari hizi haswa kupitia upanzi na uhifadhi wa mikoko

Wanawake katika kijiji cha Mtangawanda katika kaunti ya Lamu wakipanda miche ya mikoko.
Wanawake katika kijiji cha Mtangawanda katika kaunti ya Lamu wakipanda miche ya mikoko. © NRT
Matangazo ya kibiashara

Katika kijiji cha Mtangawanda, jimboni Lamu pwani ya Kenya, tunakutana na kundi la akina mama ambao kupitia mafunzo, sasa ni wakereketwa wa mazingira.

Mikoko kama bado ni michanga katika kisiwa cha Pate, kaunti ya Lamu.
Mikoko kama bado ni michanga katika kisiwa cha Pate, kaunti ya Lamu. © NRT

Licha ya changamoto mbalimbali kukiwemo dini na hata ukataji haramu wa mikoko kutokana na umuhimu wake, kinachowatia moyo ni hatua walizopiga katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, na hata cha ziada ni kufanikiwa kuchakata tena taka za plastiki ambazo ni hatari kwa ukuaji wa mikoko.

Akina mama wakiwa katika shughuli ya kupanda miche na kutoa iliyoharibika katika kisiwa cha Pate Jimboni Lamu.
Akina mama wakiwa katika shughuli ya kupanda miche na kutoa iliyoharibika katika kisiwa cha Pate Jimboni Lamu. © NRT
Vipindi vingine
  • 10:03
  • 09:59
  • 10:09
  • 09:46
  • 09:59
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.