Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA-HABYARIMANA-HAKI

Mahakama ya Ufaransa kutoa uamuzi kuhusu washtumiwa katika kesi ya Habyarimana

Hatua muhimu ya mahakama katika uchunguzi juu ya shambulio la ndege ya rais Habyarimana, ambalo linachukuliwa kuwa ndio chanzo cha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda inatarajia kuanza leo Ijumaa.

Askari wa RPF akikagua eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali,usiku wa  Aprili 6 mwaka 1994.
Askari wa RPF akikagua eneo ambako ndege ya aliye kuwa rais wa rwanda Juvenal Habyarimana ilipodondokea baada ya kudunguliwa ikiwa angani kwenye uwanja wa Kanombe, mjini Kigali,usiku wa Aprili 6 mwaka 1994. Getty/Scott Peterson
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Rufaa ya Paris inatarajia kutoa uamuzi wake ikiwa washtumiwa saba wa mauaji ya rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana, ambao ni washirika wa karibu wa Paul Kagame watafuatiliwa na mahakama nchini humo au la.

Mwaka 2018 Mahakama ya mwanzo nchini humo ilifutilia mbali kesi hiyo, ambayo ilianzishwa tangu miaka 20 iliyopita.

Kesi hii ya "mauaji na kula njama kwa ushirikiano kundi la kigaidi" ilifunguliwa nchini Ufaransa mnamo mwaka 1998, kufuatia malalamiko yaliyotolewa na familia za marubani kutoka Ufaransa, waliokuwa wakiendesha ndege hiyo ya rais Habyarimana.

Majaji wawili wa Ufaransa wa kitengo kinachopambana dhidi ya ugaidi waliokuwa wakishughulikia kesi hiyo waliamua kuachana nayo Desemba 21, 2018, "baada ya kukosekana ushahidi wa kutosha", kwa mujibu wa majaji hao ambao pia walibaini kuwepo na "hoja zinazopingana na ambazo hazikuchunguzwa" kuhusiana na ushahidi uliokusanywa.

Mawakili wa upande wa mashitaka wanataka hasa kwamba mahakama ya Ufaransa ipate ripoti ya siri ya mwaka 2003 kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai iliyoundwa kwa ajali ya Rwanda.

Rais Juvenal Habyarimana aliuawa na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira katika shambulio dhidi ya ndege yao wakati ndege hiyo ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa aw Kanombe jijini Kigali ikitokea nchini Tanzania katika mazungumzo ya kusaka amani nchini Rwanda, Aprili 6, 1994.

Baada ya tukio hilo, machafuko yalizuka, na watu zaidi ya Laki nane, wengi wao kutoka jamii ya Watutsi waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.