Tanzania yalegeza baadi ya vizuizi vya safari za ndege
Serikali ya Tanzania imelegeza marufuku dhidi ya safari za ndege za kimataifa, kwa kile mamlaka zimesema ni kutokana na uongezeko la mahitaji ya huduma muhimu.
Imechapishwa:
Hamza Johari, mkurugezi wa huduma za Ndege nchini humo amesema hilo limeafikiwa kutokana maombi ya kutaka kulegeza masharti hayo,ili ndege za kutoa hudumu muhimu kama vile usafirishaji wa dawa ziruhusiwi kupaa.
Wakati huo huo serikali ya Zambia imechukua hatua ya kufunga mpaka wake na nchi jirani ya Tanzania kuanzia leo Jumatatu kwa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Hii ni baada ya kuwa na maambukizi mengi, hususan miongoni mwa wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwenye miji ya mipaka nchini humo.
Akizungumza kwa niaba ya rais wa taifa hilo, Edgar Lungu Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya ametangaza kwamba mpaka huo utafungwa kwa muda .
Amesema kwamba hatua hiyo itatoa fursa kwa mikakati mipya ya kukabiliana na virusi hivyo kuwekwa.
Katika muda huo, amesema wafanyakazi wa uhamiaji katika mpaka huo watapatiwa mafunzo mapya ya jinsi ya kuhudumia mizigo na raia wanaoingia.